Semina ya Mchezo wa KARATE yaanza Jijini Dar es Salaam
Senpai Esther Thomas (kushoto) akipangua chudan tzuki (ngumi ya kifua) wakati semina hiyo ikiendelea.
Anafundisha kwa mifano! Shihan Okuma akishambuliwa na Jerome Sensei kama sehemu ya maelekezo katika semina hiyo
Na Daniel Mbega
SEMINA kubwa ya Shotokan Karate kwa nchi za Afrika Mashariki,
Kati na Kusini, imeanza leo hii jijini Dar es Salaam ambapo kwa mara ya kwanza
katika historia ya mchezo huo nchini Tanzania, inaongozwa na mkufunzi mkuu,
Shihan Koichiro Okuma (6th Dan), kutoka makao makuu ya chama cha
karate cha Japan Karate Association/World Federation (JKA/WF), Tokyo, Japan.
Semina hiyo – maarufu kama JKA/WF- Tanzania Southern, Central
& East African Region Gasshuku – ambayo imeandaliwa na chama cha Japan
Karate Association/World Federation-Tanzania (JKA/WF-Tanzania) ni ya nane
kufanyika ambapo kwa mwaka huu inashirikisha makarateka 45 kutoka Zimbabwe,
Zambia, Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania.
Kwa mujibu wa JKA/WF-Tanzania, semina hiyo ya wiki nzima
inatarajiwa kufikia tamati Jumamosi.
Makarateka ambao wameanza kushiriki leo hii, kutoka Tanzania
ni Jerome Mhagama Sensei, Justine Limwagu, Seberian Dagila, Said O. Kissailo, Lulangalila
Lyimma, Athumani Kambi, Mikidadi Kilindo Sensei, Marcus George, Khamis K.
Sambuki, Hamis Said Mkumbi, Selemani A. Mkalola, Christopher William, Eliasa
Mohammed, Adson Aroko Sensei, Nestory Federicko, Daniel Mbega, Willy Ringo
Rwezaura Sensei, na Shihan Dudley Mawala Sensei, ambaye alikuwa mgeni mwalikwa.
Makarateka wengine na nchi zao kwenya mabano ni Gibson
Sangweni (Zimbabwe), Robert Chisanga (Zambia), Thobias B. Rudhal (Kenya), George
Otieno (Kenya), Joshua Oude (Kenya), George Warambo (Kenya), George Okeyo (Kenya),
Florence Kieti (Kenya), Asana Mahmoud Ulwona (Uganda), Ofubo Issa Yahaya (Uganda),
Magezi Yasiin (Uganda), Wanyika Abdurahman (Uganda), Frederic Kilcher (Ufaransa)
na Koichiro Okuma (Japan).
Mkufunzi mkuu wa JKA/WF-Tanzania, Jerome George Mhagama Sensei
(5th Dan), amesema hata hivyo kwamba, tofauti na miaka
iliyotangulia, safari hii hakutakuwa na mashindano ili kutoa fursa kubwa kwa
Shihan Okuma kufundisha vyema na kuwapandisha madaraja makarateka mbalimbali
kuanzia ngazi ya Sho-Dan, Ni-Dan, San-Dan na Yon-Dan (1st – 4th
Dan).
Shihan Okuma akitoa neno kabla ya kuanza kwa semina leo hii mchana.
Shihan Okuma akijiandaa kuanza darasa leo mchana. Kushoro ni Willy Ringo Rwezaura Sensei.
Timu ya Kenya hii.
Makarateka wanapasha misuli.
Heian Shodan Kata.
Post a Comment