Zaidi ya Bilioni 4 kutumika kuwezesha wajasiriamali Kinondoni
Afisa
uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akizungumza na
Waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya Manispaa hiyo kuwawezesha
wanawake na vijana kupitia mfuko maalum ulioanzishwa na Serikali ili
kutoa mikopo kwa wajasiriamali hao ili kuwajengea uwezo kushiriki
kujenga uchumi.kulia ni AfisaUhusiano wa Manispaa hiyo Bw.Bornwell
Kapinga.
Serikali kutumia zaidi ya bilioni
4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya Kinondoni katika
Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini
Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebvastian
Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua Mhowera amesema fedha
hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana unaolenga
kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia
kukuza uchumi.
Kwa Sasa manispaa ya Kinondoni
inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye jumla ya
wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200
waliokuwepo mwaka 2013.
Wajasiriamali wanaonufaika na
fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za Kiuchumi
ikiwemo kilimo,Biasharandogondogo,Ushonaji,Ufugaji,Uvuvi,Mafundi
seremala,wasusi.
Pia Mhowera alitoa wito kwa
wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kuchangamkia fursa
zinazotokana na mfuko wa wanawake na vijana.
Kuanzishwa kwa mfuko huu katika
manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu
lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake
kwa ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.
Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadowadogo
wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana inayotolewa na
Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.

Post a Comment