Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa MAGHEMBE akutana na Mbobezi wa Picha
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akikabidhiwa kitabu cha
picha za wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba la Selous na Mtaalamu
wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross wakati alipomtembelea leo
ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha picha
za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous kinatarajiwa
kuzinduliwa leo na Mhe. Waziri ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu
, Injinia Angelina Madete, katika Hoteli ya Slip way. Kitabu hicho
kinatarajiwa kutumika kama nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa
Tanzania katika Nyanja za Kimataifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiangalia
baadhi ya picha katika kitabu cha picha za wanyamapori waliopo katika
Pori la Akiba la Selous na mara baada ya kukabidhiwa kitabu hicho na
Mtaalamu Kimataifa, Bw. Robert Ross (kushoto) wakati alipomtembelea
leo ofisini kwake Mpingo House jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho cha
picha za wanyamapori waliopo katika pori la Akiba la Selous
kinatarajiwa kuzinduliwa leo jioni katika Hoteli ambapo Kitabu hicho
kitakuwa ni nyenzo muhimu katika kutangaza Utalii wa Tanzania katika
Nyanja za Kimataifa.
Huu
ni mwonekano wa nje wa kitabu cha Picha zilizochukuliwa katika Pori la
Akiba Selous na Mtaalamu wa picha wa Kimataifa, Bw. Robert Ross,
Kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa leo na Waziri, Prof. Maghembe
ambaye atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Injinia Angelina Madete
katika hoteli ya Slipway.
Post a Comment