Wabunge Mkoa wa TANGA watoa Pole kwa Familia za Wahanga wa Mauaji
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia
,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani
Tanga mara baada ya kutembelea eneo la Zed B ambapo wamehamia wananchi
wa Mtaa wa Kibatini kulipotokea mauaji wa watu wanane kwa kuchinjwa
ambapo aliongozana na wabunge wa mkoa wa Tanga kuwapa pole wahanga wa
tukio hilo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na
kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru.
Waziri
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama
vitu vya wahanga wa tukio la mauaji lililotokea kijiji cha kibatini juzi
akiwa na wabunge wa mkoa wa Tanga kushoto ni Mbunge wa Jimbo la
Muheza,Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
Mambo ya Nchi za Nje na Ndani.
Mbunge
wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge Mambo ya Nchi za Nje na Ndani akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kutembelea eneo la Zed B ambalo wamehamia baadhi
ya wananchi walionusurika tukio la mauaji ya watu wanane waliochinjwa
juzi kwenye Mtaa wa Kibatini wilaya ya Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Pangani
(CCM)Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuwatembelea wananchi hao kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mambo
ya Ndani na Nje ,Balozi Adadi Rajabu na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM).
Mstahiki Meya wa Jiji la
Tanga,Mustapha Selebosi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
wabunge wa mkoa wa Tanga kutembelea wananchi waliohamia eneo la Zed B
baada ya kuhama makazi yao ya Mtaa wa Kibatini kutokana na kutoka mauaji
ya watu wanane waliochinjwa juzi na watu wasiojulikana.
Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimuakiwapa pole mmoja wa wafiwa katika tukio hilo la mauaji.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga,Lucia Mwiru akimfariji mmoja wakina mama ambaye mumewe aliuwawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.
Post a Comment