Header Ads

VODACOM yazindua Huduma ya Habari " PAPO HAPO " kwa Wasanii

NA RAYMOND URIO

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom, imezindua huduma mpya ya Papo Hapo, kuwawezesha wateja wake kupata habari zinazohusu wasanii mbalimbali nchini kupitia ujumbe mfupi ‘sms’ katika simu zao.

Huduma hiyo iliyozinduliwa jana, Makao Makuu ya Vodacom, jijini Dar es Salaam, itamuwezesha mteja kupata taarifa za kila anachokifanya msanii anayempenda kwa haraka zaidi.

 Meneja wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia), akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo, kawaajili ya Uzinduzi wa Huduma ya kutoa habari ya 'Papo Hapo' kwa Wasanii, kushoto ni Msanii wa Tasnia ya Maigizo, Kajala Masanja na Aunt Ezekiel. Picha zote na Raymond Urio

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema, huduma ya Papo Hapo inalenga kuwaunganisha wateja wa mtandao huo na wasanii wanaowapenda.

“Tunataka kuwaweka watu karibu na hii ni moja ya jitihada zetu  za kutumia teknolojia kurahisisha na kufanya maisha ya wateja yawe katika hali nzuri na sio kuhangaika kutafuta habari za wasanii 
wanaowapenda.

 Mkurugenzi wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uzinduzi wa huduma ya 'Papo Hapo' za Wasanii, Kulia ni Msanii katika Tasnia ya Ugizaji na Uimbaji, Zuwena Mohammed 'Shilole'.

Huduma hii itawapa uwezo wa kupata habari kwa haraka zaidi na kwa gharama ya Sh. Mia Moja, kupitia ujumbe wao mfupi ‘sms’ kwenye simu zao za mikononi” alisema Nkurlu.

NkurIu alisema Iicha ya wateja kupata huduma hiyo iliyounganishwa moja kwa moja kwa gharama nafuu, lakini mteja bado ana uwezo wa kujiondoa katika huduma hiyo.

“Tulivyowaunganisha wateja wetu katika huduma hii haina maana kuwa ndio hawawezi kujiondoa, mteja anaweza kujiondo na akaendelea kupata huduma nyingine za mtandao wetu” alisema Nkurlu.

Wasanii walioingia mkataba wa miaka miwili na Vodacem kwa ajili ya huduma hiyo ni Ali Kiba, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Kajala Masanja, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Rose Ndauka, huku Nkurlu akiongeza watasaini mikataba na wasanii wengi.

“Huu ni mchanganyiko wa wasanii wa maigizo na waimbaji, lakini tutakuja kusaini mikataba na wasanii wengine, lakini kwa kuanzia tumeanza na wasanii hawa” alisema.


Mmoja ya wasanii waliokuwepo katika uzinduzi huo Shilole alisema, amefurahshwa na huduma hiyo ambayo itasawasaidia maashabiki wao kufahamu jinsi wanavyofanya shughuli zao.

“Binafsi nina vituko vingi na mashabiki wangu watakiwa kufahamu kila ninachokifanya kama niko studio narekodi au nafanya kitu gani, hivyo kwa huduma hii itawafanya mashabiki wangu kupata habari zangu kwa haraka zaidi” alisema Shilole.

Kajala nae alisema, kuwepo kwa huduma hiyo kutafanya kuwa karibu na mashabiki wao na itawaongeza nguvu katika kufanya kazi nzuri na kuwavutia zaidi mashabiki.

No comments

Powered by Blogger.