Tanzania Kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya 6 ya Wiki ya Maji Barani Afrika
Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo. |
Akifafanua Matemu amesema kuwa mkutano huo utahusisha washiriki zaidi ya 1000 kutoka mataifa 54 kutoka Bara la Afrika na wengine kutoka nje ya Afrika.
Maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya shughuli za wadau wa sekta ya maji na umwagiliaji, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Kauli mbiu ya kongomanao hilo ni “ Kufikia lengo la maendeleo Endelevu Juu ya usalama wa Maji na usafi wa mazingira” alibainisha Matemu.
Mkutano huo utawasaidia wataalamu wa maji kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika kujadiliana kuhusu mikakati mbalimbali itakayosaidia kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya maji katika bara la Afrika.
Akizungumzia faida za Mkutano huo Matemu amesema kuwa utasaidia kufungua fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya maji na Sekta nyingine ikiwemo kukuza na Kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini hali itakayosaidia kukuza Utalii.
Post a Comment