Mfuko wa Pensheni PPF wandaa Futari kwa Watumishi wake
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio
(kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini
Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari
iliyoandaliwa na Mfuko huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza
wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari
iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam
jana Juni 17, 2016.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla
hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio,
akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati
wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo
kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016.
Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis.
Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapo pichani) wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwani mfuko
huo ni faraja kwa Watanzania na unaofanya mambo makubwa kwa lengo la kuwasaidia
wananchi.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania,
Sheikh Ali Hamis wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na uongozi wa mfuko
huo kwa wafanyakazi wake.
Alisema kuna faida kubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo
kwani watafaidika na mafao mbalimbali yanayotolewa na PPF.
Aidha Sheikh Hamis alisema kuwa ipo haja kwa watendaji wa mfuko
huo kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waendelee kujiunga na PPF.
Alifurahishwa na namna uongozi wa mfuko huo ulivyoandaa hafla ya
futari hiyo maalum kwa kuwafuturisha wafanyakazi wake na kwamba hilo ni jambo
jema kwani wafanyakazi wanafahamiana na kubadilishana mawazo.
Sheikh Hamis aliitaka jamii kuwaenzi waasisi wa taifa hili kwa
kuendelea kudumisha Amani na umoja kwani wamefanya jambo jema la kuwafanya
wananchi wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila.
Kwa mujibu wa Sheikh Hamis, PPF ni aina ya mfuko
unaowawezesha wananchi kujikomboa.
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio
aliwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki futari hiyo,ambayo imekuwa ikiandaliwa
kika mwaka na kuwashirikisha wafanyakazi wake wote.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUICO aliushukuru uongozi
wa mfuko huo kwa kuwaandalia futari hiyo.
Futari hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa PPF kutoka makao
makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo.
Post a Comment