Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo yatoa Elimu Kuhusu Simu Bandia
Kampuni
ya Tigo Tanzania leo imetangaza ofa mpya ambayo watumiaji wote wa
simu ambazo ni bandia watapata simu halisi kila watakapotembelea
duka la huduma kwa wateja la Tigo kubadilishwa simu hizo.
Mradi huu unalenga kuwawezesha
Watanzania kupata simu halisi kutokana na ukomo wa matumizi ya
simu kwa wale walio na simu feki unafikia mwisho wake.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Mamlaka ya Usimamizi wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuwa simu zote
bandia na ambazo sio za viwango vinavyokubalika ambazo
ziko katika soko la Tanzania zitazimwa kuanzia Juni 16 mwaka huu.
Akitangaza ofa hiyo Mkuu wa Vifaa wa Tigo, David
Zakaria alisema kuwa kampeni hiyo ya utambuzi imo katika mkakati wa
kampuni katika kuisaidia mikakati ya serikali pamoja na Watanzania dhidi
ya bidhaa bandia na hali kadhalika kukidhi usalama wa
mifumo ya malipo ya Tigo Pesa.
Akifafanua kuhusu ofa hiyo
kwamba kimsingi inawalenga wateja walio na simu bandia
Zakaria alisema, “Tunawataka wateja wetu kutembelea maduka Tigo ya huduma kwa
wateja yaliyopo nchi nzima kuhakiki simu zao na baada ya kuhakiki,
wote wataobainika kuwa na simu feki watapata simu halisi aina ya Itel 2100
watakaponunua kifurushi cha 22,000/-.
Zakaria alisema
ofa hiyo ni nono kwani kwa kawaida, simu hiyo huwa inauzwa kwa bei ya 30,000/-
na sasa itapatikani kwa 22,000/- tu, huku akiongeza kuwa simu hiyo itakuwa na
dakika 350 za kupiga simu bure katika mitandao yote, ujumbe wa maneno 1,000 na
MB250 za intaneti kila mwezi kwa miezi mitatu.
Post a Comment