Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi
linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee
wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam na kuwaahidi waumini
wa kanisa hilo kuwa Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo
Kibangu hadi River Side ambako itaungana na barabara ya Mandela.
Rais Magufuli ambaye
amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo iliyofanyika leo tarehe 05
Juni, 2016 amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na
waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine wa eneo la Ubungo Kibangu kwa lengo
la kujionea hali halisi.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa
lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt.
Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo
Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.
|
|
Mchungaji
wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo ‘mzee wa upako akiagana na mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuhudhuria ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo
Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru
waumini (hawapo pichani ) wa kanisa hilo la Maombezi la Mzee wa Upako.
|
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama
Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony
Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais
Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo maarufu
kwa jina la Mzee wa Upako kwa huduma
ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake
vya Mahubiri kupitia Luninga.
“Mimi ni
mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa
yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo
nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.
“Ndio maana kuna
siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za
namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa
barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto
zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha
za kutengenezea barabara hii zipo” Amesema Dkt.
Magufuli huku akishangiliwa na waumini.
Kwa upande wake
Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa
hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze kufanikisha azma ya
kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha viwanda.
|
Post a Comment