Tamasha la Vijana Kufanyika IFAKARA Mkoani MOROGORO
Kutoka kushoto ni Manoah William Waziri wa Elimu Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agnes Inocent wa YFF, James Isdore Mwenyekiti wa Msafara,Fadhiri Meta kutoka Youth can na Batseba Modest kutoka Ngao youth wakiongea katika mkutano huo na waandishi wa Habari leo 9.12.2015.
James Isdore Mwenyekiti wa Msafara akizungumzia Shughuli ya msafa kwa ujumla.
Fadhiri Meta kutoka Youth can akizungumzia jinsi Msafara ulivyopokelewa vizuri na mpaka sasa wamepata zaidi ya vijana 500 ambao wanajifunza ujasiliamali na kuibua vipaji na ubunifu mbalimbali.
Agnes Inocent akizungumzia jinsi watakavyo hamasisha wanawake wengine kujitambua na kuwa wanaweza.
Batseba Kassanga (Kulia) akitoa wito kwa vijana namna wanavyoweza kujikomboa kupitia Msafara.
Noah William akifafanua jambo kuhusiana na Msafara.
Mkutano ukiendelea........
Programu ya Msafara inayoendeshwa asasi tano za kiraia ambazo ni; YouthCAN, TYDC, DARUSO, NGAO YOUTH na Young Feminist Forum kwa uratibu wa Shirika la Oxfam, inatarajiwa kufanyika mapema kesho kutwa katika Mkoa wa Morogoro wilayani Ifakara.
Programu
inayolenga kuwahamasisha vijana kubuni njia za kujikwamua kiuchumi kupitia
wenzao waliofanikiwa, itafanyika kwa njia ya tamasha kubwa katika eneo la
Uwanja wa Taifa, Ifakara mkoani Morogoro ambapo ndani ya tamasha hilo mitaji na
motisha ya kukabidhiwa vitendea kazi itagaiwa kwa vijana wenye umri kuanzia
miaka 15 hadi 24.
Mbali na
kutoa elimu na motisha hiyo, tamasha hilo litapambwa na burudani za aina mbalimbali
huku pia kukiwa na vijana waliofanikiwa watakao wahamasisha wenzao kupitia kauli
mbiu ya Inspire, Aspire and Activate.
Post a Comment