Mahafali ya 9 ya Chuo Kikuu Ardhi Yafana, 1874 Wahitimu katika Fani Mbalimbali
Mlau (Proctor) wa Chuo Kikuu Ardhi
Prof.Joseph Lusuga
Kilonde akiongoza andamano la wanataaluma (Academic Procession) wa Chuo
Kikuu Ardhi Wakati wa Mahafali ya 9 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya (kulia) na Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof.Idrissa Mshoro wakiongoza wahitimu wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 9, mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya (katikati) na na viongozi wengine wa chuo hicho wakiwaongoza wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi na wageni mbalimbali Kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuwatunuku wahitimu wakati wa Mahafali ya 9 ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Katika fani mbalimbali wakijiandaa kutunukiwa shahada zao wakati wa Mahafari ya 9 yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Mhe. Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamivu ya Chuo Kikuu Ardhi Bw. Mnyone Ibrahim mmoja wa wahitimu 2 wa Digrii ya Uzamivu ya Chuo hicho kufuatia mada ya Utafiti aliyoifanya kuhusu Uendelezaji wa Makazi ya Gharama nafuu kwa ajili ya maisha Bora ya ya Watu wa kipato cha chini.
Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof.Idrissa Mshoro akizungumza na wahitimu wa Chuo hicho na hadhara iliyohudhuria Mahafali ya 9 ya chuo hicho kwa mwaka 2015 jijini Dar es salaam.
Juu na Chini Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi waliohudhuria Mahafali ya 9 ya Chuo hicho katika Ukumbi wa Diamond Jubilee wakifuatilia Matukio mbalimbali, Wahitimu 1874 wametunukiwa Digrii za Uzamivu ,Uzamili,Shahada na Stashahada za fani mbalimbali katika usimamizi wa Sekta ya Ardhi. Picha na Aron Msigwa-MAELEZO
Post a Comment