Fedha za Mkesha wa Amani Kuokoa Vifo vya Wajawazito na Watoto
Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste,(Katikati) ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
Wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste wakiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili ya kuzungumzia mkesha utakaofanyika Desemba 31
………………………………………………………………………………..
Na Skolastika Tweneshe-Maelezo
Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji hasa afya ya mama na mtoto.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Ask
ofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
ofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Malassy alisema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua (solar Panels) ili kuwasaidi wamama wajawazito na watoto wanaozaliwa.
“Kina mama wajawazito na watoto wanakufa mahospitalini kutokana na kukosa umeme hasa vijijini, hivyo tumeamua fedha zitakazopatikana mkesha huu tutanunua solar” alisema Malassy
Aidha Askofu Malassy amewaomba wananchi kuzidi kumuombea Rais John Magufuli katika kuliongoza Taifa la Tanzania ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi ambayo tayari imekubalika ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti huyo alitambulisha kitabu kiitwacho IJUE SIRI YA AMANI KWA TAIFA ambacho kinauzwa Sh.5000 amesema kuwa kitabu hicho kina lengo la kuelimisha thamani na jukumu la watanzania kuilinda Amani bila kujali itikadi za dini, siasa wala ukabila
Pia ameomba kwa atakaeguswa na matatizo yanayowakumba wamama wajawazito anaweza kutuma mchango wake kwa namba zifuatazo 0755202204,0719202204,0684202204.
Mkesha huo ni wa 18 tangu uanze kufanyika na mwaka huu utafanyika katika Uwanja wa Uhuru usiku wa tarehe 31 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Awamu ya Tano Mhe. John Pombe Magufuli.
Post a Comment