Wakazi wa Wilaya ya MBOGWE mkoani GEITA wapata Ujasiri wa Kutumbua Majipu
Na Krantz Mwantepele, Geita
Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na
wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana
naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi
wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya
Mbogwe mkoani Geita.
Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson
toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo
alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje
wakati yeye si kiongozi na ni jukumu la wanakijiji wote.
Katika
mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na
waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha
kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja
mkizithibithisha na vielelezo. Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka kwa
nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo kwa
uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n u k u
c h u k u a hatua.”
Baada ya maelezo hayo walitakiwa
kwenda kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na
baadhi ya maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri.
Maelezo haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18
ya Katiba.
“Kweli mazungumzo hayo yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua
Hatua alinipatia muongozo na akanipangia kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa
moja nikaonana na DC nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali kuhusu pembejeo. Ingawa
majibu aliyonipa sikuridhika nayo, lakini nilishukuru kupata nafasi ya kuongea
naye. Na kwa kweli tokea siku hiyo nikawa na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida
akitoa ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.
Ujasiri huo wenye msukumo wa ndani toka kwa mraghbishi mmoja
kwenda kwa wenzake kwa njia ya kuwashirikisha aliyopatiwa na Chukua Hatua, ndio
umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya pamoja ya wana Shenda katika kusimamia
rasilimali zao. Safari ya mwandishi katika kijiji cha Shenda ilimtia moyo sana.
Alikutana na waraghbishi toka vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe. Mkusanyiko
huu ulikuwa na watu wa kada mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya kijiji,
wazee, na wakulima. Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji
chao. Na wote kwa pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa maendeleo ya
kijiji chao.
Na kwa haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi, akajiuliza
aliyekutana na Chukua Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa makundi na wote
wanajitambulisha kama waraghbishi. Hamu na shauku yao ya kutaka
kusimamia rasilimali zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia
matumizi ya vyanzo vya mapato ya kijiji chao.
Ni miaka miwili imepita toka
wananchi hao wautoe uongozi wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa
fedha. Kwa pamoja waliongozana na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji
na mpaka ofisi ya kata na kuwakabidhi kwa polisi.
Ubadhirifu huo ulithibitishwa
na taarifa ya ukaguzi, iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili
laki tisa na elfu hamsini (2,950,000/-). Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano
wa hadhara na viongozi kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.
Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika pichaya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.
...............................
Baada ya hapo walichagua uongozi mpya; mwenyekiti na halmashauri
ya serikali ya kijiji na Mkurugenzi wa wilaya akawaletea mtendaji mpya wa
kijiji. Na huo ndio ukawa mwanzo mpya wa safari ya uraghbishi katika kijiji
hicho.
Vuguvugu hilo la mapinduzi liliongozwa na waraghbishi wapya
waliowezeshwa na Fedson wakisaidiana na rafiki yake wa karibu Abdu Haridi
ambaye pia ni mraghbishi. Habari ya kutolewa madarakani kwa uongozi
wa kijiji hicho ilirushwa pia na redio ya Kahama FM na kupelekea mkuu wa wilaya
kumtuma mwakilishi wake akaongee na wananchi wa kijiji cha Shenda.
Uungwaji
mkono huu na Mkuu wa Wilaya ni dalili kwamba yupo tayari kufanyakazi na wananchi wa kijiji cha Shenda. Yeye ni kiongozi wao na
dhahiri anawajibika kwao kama ambavyo kiongozi yeyote anayejali watu wake
angefanya. Kwa sasa wanashirikiana kwa pamoja na uongozi mpya
na mwandishi alithibitisha hivyo kwa kuwa alipata fursa ya K a
m a mwanzo mpya, wamekubal i ana kufanya ujenzi wa ofisi mpya ya kijiji.
K wa n z a wa
meanza na ujenzi wa zahanati kwa k u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi
wamekubali kuchangia, kila kaya matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a
mawe. Uhai umerudi tena na kila mtu ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo.
Lakini si hivyo tu wanataka kukamilisha pia na ujenzi wa zahanati ya kijiji.
Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano kati ya uongozi wa kijiji na
waraghbishi na wanakijiji wote kwa ujumla. “Tumekaa muda
mrefu sana bila zahanati hasa kwa ajili ya kina mama.
Ni kilometa tano kutoka
hapa mpaka zahanati ya jirani. Na kijiji chetu kama unavyokijua, hakina teksi,
labda tumbebe kwa tela la ng’ombe au punda kama huna baiskeli. Tukajiuliza
kwanini tusiiambie serikali yetu tujenge zahanati hapa karibu,”anafafanua Abdi
Haridi. Lakini si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila mwananchi
achangie mawe, achangie matofali. Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa ofisi yao
ya kijiji.
Ya sasa ipo katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo na jengo
lenyewe lina nyufa ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata kuanguka
na hapa ndio makao makuu ya kijiji.
Kwa hiyo nguvu
zao sasa ni kukamilisha hii ofisi afu ndio waendelee na zahanati ya kina
mama. Mazungumzo hayo na Chukua Hatua yalifanyika katika mfumo wa
mafunzo yaliwawezesha waraghbishi toka vijiji vya Ipoja, Shenda,
Buluha na Nyakasaluma kuanza kufuatilia na kuhamasisha wengine kufanya hivyo
pia. Si kitu kirahisi sana kuwa mraghbishi, kunahitaji
kujiamini, kujitambua na moyo wa kujitolea pia..
Katika kijiji cha
Nyakasaluma wananchi walihamasishwa na uongozi wao kuchangia pesa kwa ajili ya
ujenzi wa Zahanati na kwa kweli walichangia kila kaya ilitoa kiasi cha shilingi
za kitanzania elfu saba mia tano.
Swali la kujiuliza michango ya maendeleo ya
namna hii, inaamuliwaje? Wananchi wanahusishwaje? Je, wamefanya utambuzi wa
watu/kaya/familia uwezo walio nao? Kwa mujibu wa mraghabishi Patrick Matagale
ujenzi ulianza lakini ghafla ukasimama na walipofuatilia ikaonekana kwamba
ujenzi hautaendelea kwa madai kwamba mwekezaji wa kijiji atamalizia na wananchi
pesa wameshachangia.
“Sasa ilikuwa ni kuhoji tu kuhusu ile
pesa iliyochangwa na wananchi”, anasimulia mraghbishi Patrick. Uaminifu
ni silaha kubwa ya uongozi imara, na mara watu wanaposhindwa kukuamini kama
kiongozi, huamua kuchukua njia yao ya kutokukupa dhamana ya kuwaongoza, “Hivyo
tulichoamua kufanya kwa sasa ni kwamba hatutachangia tena pesa na badala yake
tunahamasisha watu kuchangia vitu badala ya pesa, kama walivyofanya wenzetu wa
Shenda.
Mwenye mawe, matofali, mbao na chochote kile alete,” anafafanua
mraghbishi Patrick Matagale toka kijiji cha Nyakasaluma.
Katika
kijiji cha Iponya, suala lililoibuka ni michango wanayochangishwa wananchi. Ambapo kila
kaya imetakiwa kuchangia kiasi cha shilingi za kitazania elfu sita (6,000/) kwa
ajili ya mradi wa maji wa visima virefu. Mradi huu unafadhiliwa na benki ya
dunia na una thamani ya shilingi za kitanzania milioni 221/-
Hivyo wananchi nao
wametakiwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia pia gharama za ujenzi huo na
wananchi walikubali bila kusita na kwa ujumla wao walichangia kiasi cha
shilingi za kitanzania milioni tatu (3,000,000/-). “Cha kushangaza
wananchi wameshachanga hela zao, ila mpaka muda huu naongea hakuna ambacho
kimeshafanyika.
Lakini kwenye muhadhara tulidanganywa kwamba mradi ukishaanza
Shenda na sisi pia tutaanza kufaidika, mpaka dakika hii hakuna maji,”
anafafanua Thomas Mlekwa toka katika kijiji cha Iponya.
Wananchi
wakawa wanataka kujua nini kimetokea baada ya wao kuchanga, kama anavyosimulia
mwana mama Leornada Mathias toka kijiji cha Ipoja, “Ilikuwa mishe mishe kweli,
kila siku mwenyekiti anapita katika kaya anahamasisha watu wachangie ili
tuondokane na tatizo la maji.
Ni kweli tuliitikia tukatoa michango na
tuliambiwa tukichelewa tu huu mradi unatupita. Tukafungua akaunti na fedha
zikawekwa. Baada ya hapo tukaona kimya kabisa.” Katika
mikutano ya hadhara ya kijiji iliyofanyika hapo wananchi walitaka kujua nini
kimetokea kwani fedha tayari kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu
zimeshawekwa benki.
“Kwenye mkutano watu
wakataka kujua meza imekuwaje tuliambiwa Shenda wakipata maji na
sisi pia, mbona tayari kwa wenzetu yapo. Ndio tukaja kujua kwamba hakuna mradi
wa maji. Na badala yake viongozi wanatuambia kwamba ile fedha wanaanza kuisoma
kwenye mapato na matumizi,” anaendelea kufafanua Leornada.
Na katika
muda huo wakaambiwa kwamba tayari laki nne zimeshatumika kutokana na makato ya
gharama za kuendesha akaunti. Kwa hiyo uendeshaji wa akaunti umekula mpaka sasa
kiasi cha milioni mbili na laki tatu zimebaki laki saba tu.
Hapa pana kazi
kubwa ya kufanya. Pamoja na Shenda
kuonekana kwamba kwao maji yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna
changamoto nyingi za kuwezesha kukamilika kwa mradi huo wa maji. Na waraghbishi
wapo mstari wa mbele kufuatilia nini kinachoendelea kwenye mradi huo.
Ni mradi
ambao waliomba wapatiwe na utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo
bado hawapati maji.
“Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi
wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu
tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa
ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale
limeshakamilishwa. Mashine ipo kule kwenye chanzo cha maji.
Italike
kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu. Kuna vitongoji vingine havina
gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu niambie kitakidhi wangapi?”
anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.
Gati zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi
kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na
serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara.
Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya
viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza, “Lakini
ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi.
Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara
ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji.
Imekuwaje kwa
kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara
ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza
gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye
jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia
alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya kijiji chao.
“Changamoto
niliyoanza nayo ilikuwa ni pale shule, nilipogundua kwamba mwalimu mkuu
anaitisha michango, bila kuwashirikisha wazazi. Pamoja na nafasi niliyokuwa
nayo lakini pia nilikuwa natoa elimu kwa wananchi. Nikajengewa kampeni na
kufanyiwa uhasama na mwisho wa siku nikaambiwa nafasi ya uenyekiti
hainifai, kwa sababu natoa siri. Hivyo nimebaki mjumbe tu,” katika hali ya
upole anaelezea mraghbishi Majura.
Suala lingine ambalo
limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha Bukandwe, ambaye
alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za kitanzania elfu kumi
(10,000/-) za mfuko wa afya. Alichokuwa akifanya wakati anawaandikia alikuwa
akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka. “Kama mtu katoa hela mwaka huu
yeye anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013.
Baada ya muda
akawa amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe
muda umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura Kutokana
na nafasi yake ya uraghbishi Majura ameweza kukaa na kamati ya kijiji ya afya.
Na ameishawishi kamati kuwasiliana na watu waliolipa kuandaa vielelezo vyao na
kufanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua
gani kuhusu huyo mganga. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi
wanarudishiwa fedha zao walizochanga.
Si kitu kirahisi sana
pia kufanya uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi wamekuwa wakitishiwa
tishiwa ili wasiulize ulize maswali na kuhamasisha wananchi , lakini bado
mambo yameendelea. “Sisi waraghbishi tunapata muda mgumu sana
tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti.
Tunatishiwa amani, ila na sisi
tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya mwisho ili haki yetu
ipatikane. Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane nayo katika kuweka
mambo sawa, kama hivi. Tayari tunaonekana siye wabaya kwa wale viongozi wa juu.
Kwamba sisi tunawapondea wale.
Basi sisi tunaomba waje wale wakubwa zaidi, waje
watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza kwa kujiamini mraghbishi
Abdi Haridi wa Shenda. Harakati hizi zinaungwa mkono na
mwenyekiti wa kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu
warghabishi,
“Kila siku waraghbishi tunao hapa. Fedson huwa
anakujaga hapa wanazunguka huko na kijana wake huyu hapa Haridi. Wanapita
vijiji hadi vijiji wanahamasisha.Hivyo waraghbishi wana hamasa hata mwenyekiti
ajaye atakayekuja watakuwa msaada kwake.
Manake watamuuliza tu sasa mkuu
unakwendaje hapa na itabidi uwaeleze mambo yanakwendaje. Hivyo mnapopata pesa ni
lazima umuelezee mraghbishi zinavyokwenda.” Ni mwaka sasa umepita
toka shuguli za Chukua Hatua zisimame kwa muda, ila cha kufurahisha ni
waraghbishi wameendelea na harakati za kujiletea maendeleo kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali hasa wananchi wenzao.
Na si hivyo tu wameendelea kuwatengeneza
waraghbishi wengine ambao na wanaendeleza harakati za kuleta maendeleo.
Post a Comment