Maamuzi Mabovu na Utendaji Mbaya wasababisha Wananchi Kumchukulia Hatua za Kisheria Mwenyekiti Wao
Wanafunzi katika shule ya msingi Shenda wakiwa wamekaa kwenye moja ya darasa lililosakafiwa
.................................
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na
kilio toka kwa wananchi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na
viongozi waliowachagua pasipo kuchukua hatua zozote. Ukimya huu wa wananchi
ndio unaosababisha kilio hicho kuendelea kukuwa kila siku. Ila
vilio hivi huishaga pale tu wananchi wanapoamua kwa dhati kuchukua hatua, kama
walivyofanya wananchi wa kijiji cha Shenda. Shenda ni moja kati ya vijiji zaidi ya 200
vinavyofanya kazi na programu ya Chukua Hatua mkoani Geita.
Kijiji hiki kinapatikana kata ya Masumbwe
wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita, Jumla ya wakazi 2,454 wanaishi katika kijiji
hiki wakijishughulisha na shughuli za kilimo, uchuuzi na uchimbaji wa madini.
Fredson Yaida ni mmoja kati ya waraghabishi wanaofanya kazi na program hii,
kama walivyo waraghabishi wengine yeye pia alichaguliwa na wananchi na baadaye
kuhudhuria mafunzo maalumu ya uraghabishi, “Baada ya kuchaguliwa basi tulienda
kwenye mafunzo kule Ushirombo.
Kule tulijifunza na kujengewa uwezo wa kufahamu mapato
nmatumizi, kujua vyanzo vya mapato vya maeneo tunayotoka, haki na wajibu wetu
katika kusimamia mali za umma lakini pia kuweza kuzihojia pale inapohitajika,”
anaelezea Fredson Yaida. Kwa kuwa
mraghabishi hana mamlaka ya kisheria ya kuitisha mikutano kwa ajili ya
kuwashirikisha wananchi wote kile alichojifunza, badala yake amekuwa
akitembelea vikundi mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji na kushirikishana.
Vikundi hivyo ni pamoja na Mkombozi, Jiandae na Twende na Wakati; kila kikundi kina
wastani wa wanachama 25 mpaka 30.
Akimuelezea jinsi anavyomuelewa
mraghabishi, mwenyekiti mpya wa kijiji cha Shinde, Andrea Lubango anasema,
“huyu bwana Fredson Yaida na kikundi chake wamekuwa mstari wa mbele katika ku- hamasisha
wanakijiji kujua mambo ya mapato ya kijiji chao na kuwataka kuulizia ili kusudi
waelewe zaidi.”
Wakati wa majadiliano na wanachama wa vikundi
hivyo na makundi mbalimbali ya jamii, suala lililojitokeza ni la mapato
yanayotokana na malori yanayobeba mchanga wenye masalio ya dhahabu toka
kijijini hapo.
Akielezea jinsi alivyoitoa hoja hiyo kwa wenzake Mraghabishi Fredson
anasema, “Niliwaambia jamani sasa hivi
tuelimike sasa si mnaona magari hapa yanapakia mizigo, ushuru hatuupati, hata
mapato hatusomewi imekuwaje nchi yetu hivi na tuna rasilimali na magari kila
siku yanapakia mizigo, yapo magodown mengi tu yamejengwa hapa Shenda tulikuw hatupati
hata shilingi.”
Malori hayo huja kubeba mchanga
unaokuwa umebakia kutoka mgodi wa Shenda kwenye mawe yaliyovunjwa na wenye makarasha.
Mwenye lori huja kununua mchanga huo uliobakia na kuondoka nao pasipo kijiji
kupata mapato tokana na mchanga mali huo.
Mgodi wa shenda hutegemewa kama
njia ya kujipatia kipato hususani wakati wa hali mbaya ya kilimo baadhi ya wanavijiji
huenda kuajiriwa na wamiliki wa mashimo hayo ya dhahabu. Wanakijiji huchimba udongo
kisha huchekecha ili kupata dhahabu na baada ya kuchekecha mchanga huukusanya
pembeni mwa mashimo ya dhahabu kwa ajili ya kuuza.
Fredson anasema wengi wa
vijana ndio hujishughulisha na shughuli za migodi ili kujipatia kipato. Fununu
za kuwepo kwa wawekezaji katika mgodi wa
Shenda wakawa wanajiuliza haya malori yanayopishana na shehena ya mchanga uliochanganyikana
na dhahabu pasipo wao kupatiwa taarifa yoyote uliwapa shaka na hivyo kutaka
kujua zaidi.
Kupitia mraghabishi, vikundi na wanakijiji ukawekwa mkakati wa jinsi
ya kufuatilia hivyo kupitia uhamashaji wananchi wakaanza kuongea kichinichini hatimaye
wakaamua kuchukua hatua.
Mraghabishi Fredson Yaida (wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa wanachama wa vikundi, Mwenyekiti wa kijiji (wa kwanza kulia) na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Shinde wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ofisi ya kijiji.
......................................
“Tukaanza kuhojiana sisi kwa sisi
vipi mbona magari yanasomba tu, watu wakasema tuyasimamishe yasisombe, bahati
nzuri serikali ya kijiji ikaliona hilo kwa haraka, wakawa wameitana mwenyekiti
wa kijiji na wajumbe na mtendaji wa serikali ya kijiji. Wakaliwekea mkakati wa
kulifuatilia,” anaelezea Fredson Yaida.
Kamati ya serikali ikiwa tayari imeshanusa
kilichopo mbele yao iliwalazimu kuchukua hatua za haraka kujinusuru na hasira za
wananchi, kama anavyoelezea mjumbe wa kamati ya kijiji, Makemba Kubezia,“Tukaanza
kujiuliza sisi wenyewe wa kamati ya kijiji, mh, mbona huu mchanga unatoka kwenye
mashimo yetu pasipo sisi kujua, labda hapo mwenyekiti amefanya bila kutuhusisha
serikali ya kijiji.
Baadaye basi katika ufuatiliaji wananchi wakaanza kutuhoji ikabidi tuamke kweli na kuchukua Hatua stahili,”
Hivyo kamati ya serikali ya
kijiji ikabidi imwite mwenyekiti wa kijiji ili kujua nini kinaendelea katika
shughuli hiyo na kukubaliana kulifuatilia suala hilo ofisi ya kata na baadaye
kwenda kwa mhusika (mwenye malori) ili
kujua anasomba mchanga kwa kibali kipi.
Lakini katika hali ya kushangaza aliyekuwa
Mwenyekiti wa kijiji cha Shenda John Mapoli aliwachenga wenzake na kwenda peke
yake kuonana na mtu anayeleta malori kijijini kuchota mchanga wenye masalio ya
dhahabu.
Baada ya kurudi hakuwaita wenzake wa serikali ya kijiji kuwapa
mrejesho wa safari yake. Kukawa na
maneno ya kichini chini kwamba mnunuzi humpa mwenyekiti bakshishi (rushwa) ili
apate nafuu katika bishara yake ikiwa ni pamoja na kukwepa hiyo tozo.
Iligundulika baadae kuwa hakutaka
wagundue kuwa alikuwa akipokea pesa kutoka kwa mnunuzi, kwani alikuwa
hazifikishi katika ofisi yakijiji.Kutokana na kile kilichojitokeza ikabidi uitishwe
mkutano mkuu wa kijiji uliosimamiwa na mtendaji wa kata.
Ni dhahiri wananchi hawakuwa
na imani na Mwenyekiti wao tena na hivyo kumtaka aachie madaraka na kisha
kumteua mwenyekiti wa muda, Andrea Lubango atakaye kaimu kiti hicho mpaka
uchaguzi ujao.
“Hivyo baada ya wananchi
kumuondoa tukambana na yule mwenye lori. Kwa kuanzia akatoa kiasi cha shilingi laki tano na miifuko 60 ya sementi kati ya
hiyo, 30 imetumika kwa ajili ya ukarabati madarasa mawili na mi-fuko mingine 30
itatumika kwenye ujenzi
wa zahanati, na kuna mtu kuwalazimisha.
Tatizo ni watendaji wa vijiji,” Akitoa mfano wa hali hiyo ya watendaji
wa vijiji Diwani wa kata ya Kishapu anasema, “Kijiji hiki hapa (Kishapu) kimemaliza karibu
miezi tisa bila kusoma mapato na matumizi na nimekuwa nikimtumia mtendaji wangu
wa kata kwamba waandikie wawe wanasoma mapato na matumizi.
Lakini na yenyewe
ikawa bla bla, mpaka nikalazimika kufika ofisi ya mkurugenzi badala yake akaandikiwa,
ndio akasoma mapato na matumizi,”
Kwa upande wa Kata ya Mwakipoya
mheshimwa Thabita anasema, “Watendaji wangu sio wazuri hawataki kualika
mikutano, mambo yote yamekwama kwa ajili ya watendaji.
Nimefanya mikutano
miwilitu katika kijiji cha Mwangongo na hapa Mwakipoya. Changamoto kubwa ambayo
alikumbabana nayo kwenye vile vijiji sana sana ni malalamiko kwa watendaji kwamba
hawataki kusoma taarifa za mapato na matumizi.
na hatua aliyochukua Mheshimiwa Thabita ni kupeleka taarifa hizi kwa
mkurugenzi na mkuu wa wilaya kwa hatua
zaidi.
Lakini pamoja na changa- mwingine alichukua mchanga akatuletea mifuko
15,” anaeleza Mwenyekiti wa sasa wa kijiji cha Shande, Andrea Lubango.
Kwa hakika wananchi ndio wamiliki wa kiti cha
uenyekiti na wanapoamua kuchukua kiti chao wanaweza, kama wana Shenda wangeamua
kukaa kimya na kundelea kuhuzunika na kulalamika tu pasipo kuchukua hatua hakuna
ambacho kingAewezekana Na watoto wao wangeendelea kusoma kwenye madarasa yenye vumbi
kutokana na kutokuwa na sakafu.
Hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuweza
kuhakikisha Wanashenda wanapata mapato yenye thamani sawa na mchanga
uliochanganyika na dhahabu.
Post a Comment