(Picha na Ally Daud)
Na
Skolastika Tweneshe na Mwanahamisi Matasi
Kwa mara nyingine tena,
Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 100 duniani ambazo zipo huru kiuchumi kwa
mujibu wa ripoti ya (Economic Freedom of
the World Report) ya mwaka 2015 itolewayo na umoja wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ujulikanao kama Mtandao wa
Kiuhuru wa Kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Huru lisilo
la kiserikali linalojishughulisha na uboreshwaji wa Sera za Jamii (UIPE) Bw.
Isack Danford alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Tanzania
imepanda kwa nafasi kumi katika nafasi
ripoti ya mwaka huu kutoka nafasi ya tisini na mbili katika ripoti ya mwaka
2014 hadi nafasi ya 82 katika ripoti ya mwaka 2015.
“Kwa sasa nchi yetu ya
Tanzania inaendelea kupanda katika uhuru wa kiuchumi kwa kushika nafasi ya 82 duniani na nafasi ya tatu kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki
ikiishinda nchi ya Kenya ambayo ilikuwa kinara miaka iliyopita“alisema
Danford.
Mbali na maendeleo hayo
zipo changamoto mbalimbali ambazo zinazobomoa uhuru wa kiuchumi Tanzania ni
pamoja na malipo ya ziada(Extra payment), Hongo na upendeleo, gharama
zitokanazo na urasimu na mahitaji ya kiutawala hii ni katika uthibiti wa
biashara mbalimbali za ndani ya nchi.
Pia kwenye biashara
za kimataifa masuala yanayorudisha nyuma
uhuru wa kiuchumi ni pamoja na vikwazo katika uwekezaji ,vikwazo visivyo vya
kiforodha na tofauti katika viwango vya forodha.
Kwa mujibu wa tafiti wa
watu waishio kwenye nchi zenye viwango vya
juu vya uhuru wa kiuchumi ripoti hii hupima uhuru wa kiuchumi wa nchi mbalimbali duniani kwa kutumia vigezo vitano ambavyo ni, ukubwa wa serikali, sura
ya kisheria, usalama wa mali
binafsi,fedha imara,uhuru wa kuifanya biashara kitaifa pamoja na udhibiti wa
mikopo, ajira na biashara.
Post a Comment