Serikali yasisitiza Umuhimu wa Utunzaji Nyaraka kwa Waombaji Kazi
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo. |
(Picha na Fatma Salum)
Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika kutekeleza jukumu lake la uendeshaji wa
mchakato wa Ajira serikalini imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali
ikiwemo ya matukio ya upotevu wa vyeti vya kitaaluma na nyaraka nyingine za
msingi kutoka kwa waombaji kazi.
Tunaendelea
kusisitiza na kuwakumbusha wadau wetu kwamba miongoni vya vigezo vya msingi vinavyotumiwa
na Sekretarieti ya Ajira pamoja na Waajiri ili kujua kama muhusika anayeomba
kazi ana sifa na vigezo vinavyotakiwa katika nafasi husika ni pamoja na kuwa na
vyeti vya kuhitimu taaluma husika.
Takribani
waombaji kazi 256,928 wamekosa fursa ya kuitwa
kwenye usaili ili kuweza kuajiriwa Serikalini kutokana na sababu mbalimbali
zikiwemo za kutokuwa na vyeti vya kitaaluma, kutozingatia vigezo vya tangazo la
kazi, kuomba nafasi ya kazi ambayo mwombaji hana sifa zinazokidhi nafasi hiyo.
Kumekuwa
na tatizo kutoka kwa baadhi ya Waombaji kazi wengi kutotambua umuhimu wa
kutunza Vyeti vyao vya kitaaluma na nyaraka nyinginezo kama vitambulisho, vyeti
vya kuzaliwa, hati ya kusafiria pamoja na barua za utambulisho.
Imekuwa
ni kawaida kwa waombaji kazi wanaowasilisha maombi ya ajira kukuta baadhi yao hawana
vyeti kwa maelezo kuwa vyeti/cheti kimepotea/kimeibiwa, kimeungua, kimeliwa na
panya, kiliingia maji ya mafuriko na baadhi yao kutunziwa vyeti na wazazi wao
kama ''Custodian'' wao wa kuhifadhi vyeti ama nyaraka husika.
Baada
ya kukutana na changamoto hizi, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utambuzi ili waombaji kazi wasio na vigezo
wasiweze kupata fursa ya kuajiriwa katika Utumishi wa Umma. Hii inatokana na
sababu kwamba kuwaajiri watu wasio na sifa katika Utumishi wa Umma kuna athari kubwa
katika maendeleo ya Nchi yetu na ina athari kwa jamii yote ya Watanzania.
Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwasisitizia wadau wake hususani waombaji kazi kuwa ni muhimu
wakatambua vyeti ni ajira, vyeti ni maisha, vyeti ni utambulisho na
uthibitisho.
Kwa kuwa hakuna anaeweza kuajiriwa serikalini bila ya kuwa na vyeti halisi na halali maana Serikali inaendesha mchakato wa Ajira kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na si vinginevyo.
Hivyo ni vyema wakavihifadhi katika sehemu iliyo salama ili kuvitumia pindi vinapohitajika na kwa wale waliopoteza, kuibiwa, kuungua wakatoe taarifa kwa mamlaka husika ili waweze kujua taratibu za kufuata ili kuweza kuendelea kupata huduma katika mamlaka mbalimbali.
Kwa kuwa hakuna anaeweza kuajiriwa serikalini bila ya kuwa na vyeti halisi na halali maana Serikali inaendesha mchakato wa Ajira kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na si vinginevyo.
Hivyo ni vyema wakavihifadhi katika sehemu iliyo salama ili kuvitumia pindi vinapohitajika na kwa wale waliopoteza, kuibiwa, kuungua wakatoe taarifa kwa mamlaka husika ili waweze kujua taratibu za kufuata ili kuweza kuendelea kupata huduma katika mamlaka mbalimbali.
Aidha, chombo hiki kitaendelea kukagua nyaraka zinazowasilishwa na waombaji kazi ili kubaini wale wote
wasiokuwa na sifa stahili pamoja na wanaotumia vyeti vya kughushi kwa ajili ya
kupata kazi serikalini ili kuhakikisha kuwa watu wa namna hiyo hawapati nafasi
ya kuingia katika Utumishi wa Umma.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma. 23 Desemba, 2015.
Post a Comment