Naibu Waziri wa Afya Dkt HAMIS KIGWANGALA afanya Ziara ya Kushtukiza Hospitali za Rufaa Mikoa ya LINDI na MTWARA
Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Damasiana Msalla akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea kwenye wodi za hospitali wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mkoa wa Lindi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea wodi za hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.Katikati ni Mganga wa Meno na Kinywa katika hospitali hiyo, Dkt. Hussein Athumani.
Mtaalamu wa Tehama katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Abdallah Kivurugo akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) namna wanavyomsajili mgonjwa anapofika hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akihoji jambo kwenye chumba cha mapokezi katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia).
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akionesha kombe la mshindi wa pili kwa utoaji wa huduma bora Tanzania kwa mwaka 2015 kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelekezo kwa wahudumu wa afya wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea wodi za wagonjwa wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kulia ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma ya bima ya afya katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara. Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maelezo kutoka kwa Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Getrude Mangosongo (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) alipotembelea wodi ya akinamama wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiwasili katika jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitembelea maeneo ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa ndani ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akitoa maelekezo baada ya kutembelea jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbiji.
Post a Comment