Kampuni ya TIGO yatoa Dola 40,000 ili Kuendeleza Miradi ya Wajasiriamali na Jamii
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam leo. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda.
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam leo. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda.
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam leo. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni ya Tigo ikishirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Reach for Change wametoa jumla ya dola 40,000 kwa washindi wawili wa shindano la ubunifu kwa wajasiriamali wanaotumia teknolojia ya kidijitali. Kila mshindi amepewa dola 20,000.
Shindano hilo ambalo ni la nne tangu lilipoanzishwa mwaka 2012, lina lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanaobuni miradi ya teknolojia ya kidijitali inayosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
Washindi wa mwaka huu ni Neema Shosho ambaye kwa kupitia kampuni yake ya Afya Slices, amebuni mfumo wa teknolojia ya kidijitali unaotoa taarifa kuhusu lishe kwa watoto na Bihage Edward, aliyebuni mradi wa kutunza vifaa vya elimu kidijitali unaosaidia kutokomeza ajira kwa watoto na kusambaza taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia simu za mkononi na kutengeneza programu ya Mp3 mahsusi kwa kutoa uelewa kuhusu ajira kwa watoto kwa jamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev alisema ni furaha kubwa kwao kuwatangaza washindi wa mwaka huu wa shindano la ubunifu la Tigo Digital Change-Makers.
Alisema kwa muda wa miaka minne sasa shindano hili limewanufaisha zaidi ya watoto 10,000 nchini na tunaamini kuwa ongezeko la washindi wawili litaleta mabadiliko zaidi kwa watoto na kusaidia kuifanya Tanzania kuwa mahala pazuri pa kuishi na kwamba maisha ya kidijitali yanakuza teknolojia yenye mawazo ya kuleta mabadiliko endelevu.
“Teknolojia ya kidijitali haibadilishi tu jinsi tunavyofanya biashara ila pia inasaidia kukuza biashara barani Afrika na vilevile kuleta mapinduzi ya jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kijamii kwa ujumla”, alisema Berdiev.
Huu ni mwaka wanne ambapo Tigo na shirika la Reach for Change wanazindua washindi wa shindano hili ambapo washindi huchujwa kutoka kwenye washindani vijana ambao wana mwamko wa kubuni miradi inayotumia ya kiditali ili kutatua matatizo mbalimbali ya vijana na watoto katika jamii ya Watanzania.
Ofisa mkuu huyo wa biashara alisifia kazi mbalimbali za washindi waliotangulia na kuwatia moyo wengine ili waendelee kubadilishana mawazo.
“Tumepata mafanikio makubwa sana katika kuwapa msukumo wajasiriali-jamii. Kwa sasa tunasasidia waleta mabadiliko saba ambao kati yao, watano wana miradi inayoendelea.

Post a Comment