Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki
kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya
usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa
Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo
ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na
Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 za uhuru wa
Tanzania Bara.
Akizungumza
na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais
amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni
wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.
“Haya
makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha
hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema MHe. Samia.
Alielezea
kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo
alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za
mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.
Makamu
wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni
michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na
kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa
na elimu bora.
Pamoja
na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa
Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya
DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar
es salaam
|
Post a Comment