|
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka Australia kwa
mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Peter Cosgrove. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea
na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi
Meck Sadik baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 akitokea Australia
alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Peter Cosgrove. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa
Jumamosi Agosti 1, 2015 akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko
rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter
Cosgrove. |
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhani
Madabida alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015
akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali
kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove. | |
......................................................................
Akiwa nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo
na Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa
kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa Katiba
nchini Tanzania.
Rais Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji
wake Gavana Mkuu wa
Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa
wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini
na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika kutokana na kupata gesi.
Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta,
yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na tafiti
mbalimbali katika Kilimo.
Rais Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari
wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa
alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini
Tanzania na Dunia kwa ujumla.
Post a Comment