Wadau wa Korosho Wazitaka Halmashauri Kutenga Maeneo ya Viwanda
Kikao
cha wadau wa zao la korosho kimezitaka halmashari za mikoa Mitano
inayolima zao hilo kutenga maeneo ya ujenzi wa viwanda pamoja na kuingia
ubia na sekta binafsi.
Hiyo ni Katika kuunga mkono sera za serikali ya awamu ya Tano inayotaka kuwa na Tanzania yenye Viwanda.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichohudhuriwa na wakuu wa
mikoa Mitano inayolima korosho nchini, mkuu wa mkoa wa Tanga Martin
Shigela, amesema namna bora ya kuboresha soko la zao hilo ni kuwa na
viwanda vya kutosha vya kubangua korosho.
Rajabu
Ng'onoma na Yusufu Nanila ni Wenyeviti wa vyama vikuu vya Ushirika
kutoka katika mikoa ya Pwani na Mtwara wameeleza azma yao juu ya ujenzi
wa maghala ya kuhifadhia korosho, huku wakiiomba Bodi ya Korosho Nchini
CBT kufanya Jitihada za ujenzi wa viwanda.
Kikao
hicho kilichowakutanisha wadau wa zao la korosho ikiwa ni pamoja na
wakuu wa mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Ruvuma na Tanga kimejadili
mafanikio na changamoto zilizojitokeza katika uendeshaji wa msimu wa
korosho nchini kwa mwaka 2016/2017.
Post a Comment