Header Ads

Wanahabari na Askari wa Jeshi la Ulinzi Waliopanda Mlima Kilimanjaro Wakabidhiwa Vyeti


Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwemo Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Waandishi wa Habari wakishuka baada  ya kupanda mlima huo kwa siku sita.Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Witara (Mwenye fimbo mstari wa mbele) na Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ardhini (JWTZ) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipokea Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro walipofika katika lango la Marangu,Kippi akisalimiana na Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu.
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA.
Baadhi ya Washiriki wa changamoto ya upandaji Mlima Kilimanjaro baada ya kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Star Tv ,Ramadhan Mvungi baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Clouds Media Group ,Kilimanjaro na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini ,Dixon Busagaga baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi ,Arusha ,Zulfa Musa baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari akiwa ni miongoni mwa wasicha wawili waliofika kileleni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mtanzania ,Arusha,Eliya Mbonea baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.


No comments

Powered by Blogger.