PPF yaandikisha Mamia ya Boda Boda Kwenye Mpango wa " WOTE SCHEME "
Baadhi ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pnsheni wa PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, Novemba 7, 2016.
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.
Na KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya
kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta
rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa
usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya
Temeke, walijiunga na mpango huo.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7,
2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa
Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.
Akizungumza
baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu
Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda,
litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo
itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.
“Tunatoa
wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda,
machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima
ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius.
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Rubamande Ratifa Ally.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilaya ya Temeke, ASP, Solomon Mwangamilo.
Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP_, Theopista Malya.
Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Mkuu wa Kituo cha Polisi, (OCS), cha Mabasi ya Mkoa, Ubungo Bus Terminal, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP), Sarah Bundala.
Polisi wa usalama barabarani wakiingia kwa maandamano kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga.
Askari wa usalama barabarani akiyaelekeza magari yaliyoshiriki kwenye maanadamano siku ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam, viwanja vya Mwembe-Yanga.
Waendesha Bodaboda wakiwasili kwa maandamano kwenye viwanja hivyo.
Mwanachama mpya akisajiliwa kujiunga na Wote Scheme.












Post a Comment