Header Ads

MTV EMA Kumkabidhi AliKiba Tuzo ya BEST AFRICAN ACT, Iliyotolewa Kimakosa Kwa Wizkid

MTV Europe music Awards 2016 iliyofanyika weekend iliyopita ambapo Mtanzania mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba alikua akiwania tuzo ya BEST AFRICAN ACT.

Kwenye Kipegele hicho cha Tuzo hiyo  aliyetangazwa kuwa mshindi ni Mnigeria Wizkid.

Pamoja na kwamba Wizkid alitangazwa mshindi, mtandaoni ilikua inaonyesha Alikiba ndio anaongoza kwa kupigiwa kura nyingi.

Kutokana na sintofahamu hiyo watu wakaanza kuuliza kwa nguvu imekuaje Ushindi huo kupewa asiyestahili?

 Taarifa za Uhakika Kutoka Kwenye Menejimenti ya Alikiba ni kwamba wametumiwa taarifa na MTV EMA kwamba kuna kosa lilitokea lakini wamerekebisha na kumfikishia taarifa Wizkid kwamba tuzo haikuwa yake hivyo itachukuliwa na kupewa Alikiba.
  
                                                                                                                         Source Millard Ayo

No comments

Powered by Blogger.