Header Ads

Jamii yaaswa Kufanya Kazi kwa Uadilifu ili Kujijengea Heshima

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa akizungumza katika hafla fupi ya kumkabidhi tuzo na kumvisha nishani Dkt. Fredrick Kigadye aliyotunukiwa na Baba Mtakatifu Papa. Francis  mapema wikiendi hii, Kushoto ni Mhadhama Kardina Polycarp Pengo, Dkt Fredrick Kigadye na Mkewe.
.............................

Jamii imeaswa kufanya kazi kwa uadilifu, uaminifu, weledi na uzalendo wa hali ya juu ili wapate kuheshimika na kuthaminiwa na jamii zinazowazunguka kwa kutambua mchango wao katika kuendeleza jamii.

Hayo yamesemwa na Mhadhama Kardinali Polycup Pengo wakati wa hafla ya kumkabidhi nishani ya Benemerenti  (Anayestahili), Dkt. Fredrick Kigadye, ambayo utolewa na Baba Mtakatifu kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kulitumikia Kanisa na jamii kwa ujumla jana Jijini Dar es Salaam.

“Ni vyema tukatambua ya kwamba kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio mahali pepote pa kazi na katika maisha yetu ya kila siku”. Alisema Kardinali Pengo.

Kwa upande wake Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa masema kuwa Dkt. Kigadye amekuwa mtumishi wa wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa muda wa miaka 35 huku akifanya kazi katika Idara ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mafanikio makubwa.

Ameonesha ni namna gani watu tunapaswa kujitoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na taaluma tulizo jaaliwakuwa nazo hii inatia moyo sana. Aliongeza Askofu Ngalekumtwa.

Akizungumzia Tuzo hiyo aliyopewa na Baba Mtakatifu Papa Francis, Dkt Kagadye amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kubwa na wathamani kwa kupewa tuzo ya heshima na kiongozi mkubwa duniani nakuongeza kuwa tuzo hiyo inamuongezea chachu ya kuishi katika misingi imara ya maadili na weledi.

Mhadhama Kardinali Polycarp Pengo akimkabidhi hati yenye ujumbe maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Papa. Francis Dkt. Fredrick Kigadye wakati wa hafla ya kumkabidhi tuzo aliyetunukiwa kufuatia mchango wake mkubwa katika kulitumikia Kanisa Katoliki kupitia Idara ya Afya chini ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) mapema wikiendi hii, Kulia ni Mke wa Dkt. Kigadye akishuhudia tukio hilo.

Dkt. Fredrick Kigadye akitoa neno la shukrani kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kwa kutambua mchango wake katika jamii na kanisa kwa ujumla.

No comments

Powered by Blogger.