Header Ads

TANZANIA yafanikiwa Kupunguza Vifo vya Watoto Chini ya Miaka Mitano

Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,akihutubia mkutano wa 69 wa  afya duniani unaoendela nchini Geneva-Uswisi.
..............
Mwandishi maalum-Geneva
Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto  Ummy mwalimu  wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.

Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua  katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia  vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000

Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.
Waziri wa afya Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kushoto akiwa na waziri wa afya Zanzibar Mhe.Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa shirika la afya duniani(WHO),nyuma yao ni katibu mkuu wizara ya afya Tanzania bara dkt.Mpoki Ulisubisya.
Waziri Ummy Mwalimu wakifurahia jambo kwenye mkutano huo pamoja na viongozi wengine walioshiriki mkutano huo.

No comments

Powered by Blogger.