Header Ads

Serikali yashauri Uanzishwaji wa Chama cha Mbio za Magari Kitaifa


Frank Shija-WHUSM

Serikali imetoa wito kwa wadau wa mchezo wa mbio za magari kuanzisha Chama cha Mbio za Magari kitaifa ili kurahisisha uratibu na kuongeza ufanisi wa masuala yote yanayohusu mchezo wa mbio za magari.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  wakati wa ufungaji wa mashindano ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally 2016 jana wilaya Bagamoyo.

Nkenyenge amesema kuwa kwa kuanzisha Chama cha mchezo wa mbio za magari kutarahisha uratibu wa shuguli za vilabu vya mchezo huo na hata kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na wadau wa mchezo huo.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akiongea na washiriki wa Mbio za Magari za Alliance Auto MMSC Rally zilizofanyika Wilayani Bagamoyo jana na kuwasihi kuanzisha Chama cha kitaifa kitakachosimamia mchezo huo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akiwakabidhi zawadi ya kikombe washindi wa pili wa Mbio za Magari za Alliance Auto MMSC Rally Dharam Pandya (katikati) na Manmeet Singh kutoka Timu ya Puma Energy.
.................

“Natoa wito kwa wadau wa mchezo huu ili muweze kufanikiwa zaidi anzisheni Chama cha Kitaifa kitakacho kuwa daraja la kushughulikia masuala yote yahusuyo mcheo huu kwa matiki hiyohiyo nawakaribisha Wizarani ofisi zipo wazi” Alisema Nkenyenge.

Aidha ametoa rai kwa wadau wa mchezo huo kuangalia namna watakavyoweza kuufikisha mchezo huo katika ngazi za chini zaidi ili vijana wengi waweze kushiriki.

Naye mratibu wa mashindano hayo kutoka Mzizima Motor Sports Club Bi. Hidaya Kamaga ameishukuru Serikali kwa kukubali kushiriki mashindano haya kama mgeni rasmi.

Kamaga alisema kuwa amesikia wito wa Serikali na wako tayari kukaa pamoja ili wapate muongozo wa namna ya kuanzisha Chama cha Mchezo wa Mbio za Magari hapa nchi.

Kwa upande wake  mshindi wa kwanza wa mashindano hayo Jamil Khan amemeshukuru kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo pamoja na kukumbana na changamoto ya kuzimikiwa na gari kabla ya kufika kituo cha mwisho hali iliyowalazimu kuendelea na mashindano kwa kusukuma gari hadi mwisho wa kituo.

Khan ameongeza kuwa ushindi aliopata umempa faraja na kuahidi kuendelea kuhamasisha jamii inayomzunguka kujifunza mchezo wa mbio za magari kwani ukiuelewa ni kama michezo mingine.

Ameongeza kuwa mchezo huo umeendelea kupata mashabiki hivyo ni dalili njema kuwa mchezo huu umeanza kukua hapa nchi.

Mashindano ya mbio za magari za Alliance Auto MMSC Rally 2016 mzunguko wa Tatu yamezaminiwa  yameratibiwa na Klabu ya Mzizima Motors ya jijini Dar es Salaam na kufanyika wilayani Bagamoyo.

No comments

Powered by Blogger.