Header Ads

Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha lafanyika Mjini MOROGORO

be1Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akitoa neno la shukrani mjini Morogoro, baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu ijayo.
be2Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Mali za Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ezra Msanya, akijibu maswali ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
be3Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa wilaya hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
be4Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (wa nne kutoka kushoto) akiungana na wafanyakazi wanaounda Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kuimba wimbo wa mshikamano daima, wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Mjini Morogoro Mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
be5Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mkutano uliopitia bajeti ya Wizara hiyo na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
be6Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawako pichani) mjini Morogoro, ambapo amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kufanyakazi kwa bidii na kuacha mazoea ili kutimiza malengo ya kukusanya mapato na kusimamia matumizi yake kikamilifu.
be7Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
be8Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
be11Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, baada ya kuzindua rasmi Baraza Jipya la wafanyakazi wa Wizara hiyo Mjini Morogoro mwishoni mwa juma.
be12Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akiagana na katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John Ndunguru, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Baraza jipya la Wafanyakazi wa Wizara hiyo mjini Morogoro Mwishoni mwa juma.

No comments

Powered by Blogger.