Header Ads

Profesa MAKAME MBARAWA awataka Wakandarasi Kuunganisha Nguvu ya Pamoja

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema Serikali itaweka mazingira wezeshi ili kuwawezesha Makandarasi wazawa kupata miradi mingi ya ujenzi wa miundombinu ya nchini.

Akifunga mkutano wa siku mbili wa Makandarasi Profesa Mbarawa amesema, Serikali itatenga miradi mikubwa maalum kwa ajili ya Makandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo.

“Kazi yenu ni moja tu ni kuwajengea watanzania miundombinu iliyo bora iliwafikie uchumi wakati ifikapo 2025”, amesema Prof. Mbarawa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi nchini (CRB), Eng. ConsolataNgimbwa, akisoma maazimio ya mkutano wa siku mbili wa Makandarasi kuhusu kuwajengea uwezo makandarasi wazawa, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akikabidhi cheti kwa mmoja wa Makandarasi waliofanya vizuri katika mkutano wa siku mbili wa kuwajengea uwezo Makandarasi wazawa, jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.