Header Ads

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA afanya Mazungumzo na Wawekezaji wa Umeme wa Gesi Kutoka JAPAN

4788 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe wa kampuni hiyo  ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 9, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji  baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza  kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini, Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na viongozi hao  ofisini kwake  jijini Dar es salaam May 9, 2016. 

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments

Powered by Blogger.