Header Ads

Serikali yakipiga Faini Kiwanda cha Bia cha SERENGETI

Na Mwandishi wetu, DSM

Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira Nchini(NEMC)baada ya kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya mwaka(2004)na kanuni zake.  
        
Uamuzi huo umefikiwa baada ya  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko kutoka kwa wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha uchafuzi wa mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha  usalama wa afya zao,ambapo ilimlazimu naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza  kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi kutoka Baraza la usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu huo.  
                 
Mh.Mpina  ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na kurekebisha miundo mbinu hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji maji machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya inayohatarisha afya  za wakazi wa chang'ombe wilaya ya temeke.                

Naibu Waziri Wa nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Afisa mazingira wa kiwanda cha serengeti Bw.Simon Peter mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo.   
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu ni mbunge wa Temeke (CUF) Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali za kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.                       
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho kinavyochuja maji kwa njia ya kisasa kabisa kwa ajili ya matumizi na uzalishaji kiwandani hapo.

No comments

Powered by Blogger.