Header Ads

Rais Mstaafu JAKAYA KIKWETE atembelea Daraja la Mwalimu Nyerere, KIGAMBONI

 Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo.

 Msafara wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ukipita kwenye daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, alipokagua daraja hilo leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiangaza mandhari ya darala la Nyerere alipokagua daraja hilo leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimuuliza jambo,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga (kulia), wakati akikagua daraja la Nyerere leo Kulia kwake ni Mama Salma Kikwete.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu kwenye daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakitembea kwenye daraja hilo leo. ushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipita eneo ambalo magari yatakuwa yakilipia ushuri, alipokagua daraja la Nyerere, leo.

 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama moja ya  ofisi zitakazotumiwa na magari kulipia ushuru wa kutumia daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu, alipokagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula,  kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula,  kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kulia ni Mama Salma Kikwete.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipanda ngazi kwenda kwenye ofisi za Utawala unaosimamia utoaji huduma za daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo.

 Dajala hilo la Nyerere na barabara zake linavyoonekama.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo. Kushoto kwa Jkk ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maneno ya shukurani kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete kuondoka baada ya kukagua Daraja la Nyerere leo. Daraja hilo ambalo lilianza kujengwa wakati Kikwete anamalizia awamu ya mwisho ya uongozi wake wa Urais, limefunguliwa hivi karibuni na Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli baada ya kukamilika. 

PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO 

No comments

Powered by Blogger.