Header Ads

Mamia Wamzika ANDREW NICKY SANGA ( KING DREW ) Mjini Dodoma

Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Enzi za Uhai wake.

Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga (King Drew) ukiwa unawasili katika uwanja wa Mashujaa kwa ajili ya Ibada na Kutoa kutoa Heshima za mwisho.

Ibada ikiwa inaanza Baada ya Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga kuwasili.

 Kwaya wakiwa wanaimba wimbo wao wakati wa kujiandaa na ibada.

Familia,Ndugu wa karibu, pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Serikali wakiwa katika ibada ya kumsindikiza Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga.

Mmoja wa Marafiki wakubwa wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Victor Mponzi akiwa anasoma Historia na wasifu wa Marehemu.

Mmoja wa Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa anatambulisha  wageni.

Mmoja wa wageni aliyetambulishwa na alikuja na Mwili wa Marehemu kutoka Nchini Marekani.
Huyu ni Rafiki yake sana na Marehemu Andrew Nicky Sanga ambaye anatoka Marekani na alikuja pamoja na Mwili akitoa salamu zake za Rambirambi kutoka Houston.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akitoa salamu zake za rambirambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.

Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi akiwa anatoa salamu za Rambirambi na kueleza namna alivyo mfahamu Marehemu Andrew Nicky Sanga.

Mh. Mbunge wa Viti maalum akitoa salam za rambirambi na kusisitiza upendo kama aliokuwa nao mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga.

Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akitoa neno la Mungu la wakati wa Ibada ya kuaga Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga.
 Ndugu ,Jamaa na Marafiki wakiwa katika ibada ya Mazishi ya  mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga uwanja wa Mashujaa.
 Baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu.

 Wadogo wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakiwa wanamuaga mpendwa wao.

 Mbele ni moja ya marafiki wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga aliyetoka Marekani akitoa heshima za mwisho.

 Baba wa Mzazi mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akitoa heshima za mwisho.

 Mbunge wa Mikumi Mh. Joseph Haule akitoa Heshima za mwisho.

 Baba wa Marehemu Andrew Nicky Sanga akitoa heshima zake za mwisho kwa mwanae mpendwa.

 Mzazi mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa na Mtoto wao mpendwa Zoe wakitoa heshima zao za mwisho.

Watumishi wa Mungu wakiongozwa na Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani  wakitoa neno la Baraka kwa Marehemu Andrew Nicky Sanga.

 Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakitoa Heshima zao za mwisho.

 Msafara ukielekea Makaburini.

 Mwili wa Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ukihifadhiwa katika nyumba yake ya Milele.

 Umati wa watu wakiwa Makaburini kwa ajili ya Mazishi.

 Mh. Joseph Mbilinyi na Mh. Joseph Haule wakiwa Pamoja na Marafiki wengine wa Marehemu Andrew Sanga wakiwa Makaburini.

Mama mzazi wa Marehemu Andrew Nick Sanga akiwa anaweka Shada la Maua.

 Baba Mzazi wa Marehemu Andrew Nicky Sanga na Mke wake wakiwa wanaweka Shada la maua.

 Mtoto wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wa katikati akiwa anaweka Shada la Maua.

 Mzazi Mwenzake na Marehemu Andrew Nicky Sanga akiwa anaweka Shada la Maua.

 Victor Luvena akiendelea kusoma utaratibu wa kuweka mashada.

 Wazazi wa Mzazi mwenzake na Andrew Nicky Sanga wakiweka Shada.

 Wadogo zake na Marehemu wakiweka Shada la Maua.

 Mh. Joseph Mbilinyi akiweka Shada la Maua.

 Marafiki wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga waliokuja na Mwili kutoka Marekani wakiweka shada la Maua.

 Marafiki wakubwa wa Marehemu Andrew Nicky Sanga wakiweka shada lao.

 Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akiweka Shada.

 Dkt. Sanga akitoa salamu za Shukurani kwa niaba ya Familia.

 Baba Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani akisoma neno la kufunga ibada.

 Marafiki wa Andrew Nicky Sanga wakiwa katika Picha ya Pamoja baada ya Mazishi.

Kaburi la Marehemu mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga Baada ya Mazishi.

Kama kawaida wadau wa Kutwanga Foto walikuwepo wa kutosha
Picha zote na Fredy Njeje.

No comments

Powered by Blogger.