Header Ads

Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii yatembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road

Kamati ya Bunge ya Kudumu Huduma za Maendeleo ya Jamii mapema leo Aprili 5.2016 imetembelea Taasisi ya Saratani Ocean Road na kujionea uendeshaji unaoendelea katika taasisi hiyo ikiwemo pia kuangalia jengo maalum litakalowekwa mitambo ya mionzi ya taasisi hiyo.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba (Mbunge) pamoja na wajumbe mbalimbali wa kamati huku wakibaini changamoto ikiwemo ukosefu wa dawa zinazoikabili taasisi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Julius Mwaiselage katika taarifa yake kwa Kamati hiyo aliweza kubainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili Ocean Road ikiewemo suala hilo la madawa na bajeti wanayoomba Serikali kwani uendeshaji ni mkubwa na kiwango wanachokipata ni kiasi wastani katika maobo yao hayo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla aliweza kutoa maelezo ya Wizara yake hiyo ya Afya namna walivyojipanga kusaidia taasisi hiyo huku akiahidi kuyashughulikia matatizo yote kadri inavyowezekana.

Aidha, Wananchi wakiwemo ndugu wa wagonjwa wanaouza wagonjwa wao waliweza kumvamia Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kwa lengo la kutaka kutatuliwa kero zao hasa suala la ukosefu wa dawa Hospitalini hapo ambapo walimuomba atatue tatizo hilo haraka.

Wananchi hao licha ya kupongeza huduma zitolewazo Hospitalini hapo na taasisi hiyo, tatizo lao kubwa ni ukosefu wa dawa kwani hali imekuwa ni ngumu kwa muda mrefu kwa wao kutafuta dawa nje ya taasisi hiyo na huko wanapozipata ni kwa bei kubwa.

Tazama tukio hilo: 

DSC_9652Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage (katikati) akiwa na wajumbe wa Bunge kamati ya Maendeleoya Jamii walipotembelea jengo jipya la taasisi hiyo linalojengwa kwa ajili ya kufunga mashine za mionzi.

DSC_9658Mbunge Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEA, Mh. Joseph Mbilinyi 'Sugu (Kulia) akiwa na wajumbe wengine wakitoka katika kuangalia jengo maalum linalojengwa kwa ajili ya kufungwa mashine za mionzi za kupimia ugonnjwa wa saratani.

DSC_9661
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiingia katika jengo la taasisi hiyo ya Ocean Road..

DSC_9668
Wajumbe wa Kamati ya Bunge wakiendelea na kikao hicho.

DSC_9682
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage akisoma taarifa ya taasisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

DSC_9686
Wajumbe wakiuliza maswali juu ya mwenendo wa taasisi hiyo.

DSC_9693
Kikao hicho kikiendelea..

DSC_9697
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu mawali hayo yaliyoulizwa Wizara yake.

DSC_9701
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya kina juu ya maswali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii..

DSC_9729Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na watendaji wa kuu wa taasisi hiyo muda mfupi baada ya kuagana na Naibu Waziri Dk. Kigwangalla (hayupo pichani).

DSC_9735
Wananchi wakimsimamisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla kijibu kero mbalimbali katika taasisi hiyo ya Ocean Road.

DSC_9737 DSC_9756Wananchi wakimuuliza mawali Naibu Waziri juu ya kero wanazokabiliana nazo katika taasisi hiyo wanapofika kupatiwa matibabu.

DSC_9764
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akijibu akitoa majibu kwa wananchi hao ambao wanapatiwa matibabu na wengine walifika kuangalia ndugu zao wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo ya Ocean Road.

DSC_9778Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (katikati mwenye suti) akikatiza mitaa ya Ocean Road kurejea Ofisini kwake Wizara ya Afya baada ya kumaliza majukumu yake ya kikazi ikiwemo kuambatana na Kamati ya Bunge Huduma za Maendeleo ya Jamii iliyotembelea katika taasisi hiyo ya Ocean Road.

DSC_9780
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati mwenye suti) akirejea kwa miguu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kuelekea Wizarani kwake kwa miguu... 

(Picha zote na Andrew Chale)

No comments

Powered by Blogger.