Semina ya Kuwanoa Wadau wa Sekta ya Sanaa, yafanyika Jijini Dar es Salaam
Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana
na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo
yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii
iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta
hii.
Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama
Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k....
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4fyUCGXOhk4TNqDj7qzrdbVEmaQg2JbKjNssMXIu5V1hN5Q-B7wVn5SI8kxWmzb1XMxqKfW6TJyBReUC3qkRCqUZCDulNdjMXROg8QdYEhM8FLYhlAmNwT-KkaLggUmR-6ZAHtMdc3vc/s640/c13.jpg)
Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya
Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt
Sadaka Gandi.
Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference &
Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu
wa kazi za sanaa na taratibu zake.
Ms Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa
kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii
aliyesajiliwa.
Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo,
Habari, na Wajasiriamali mashughuri.
Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya
za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.
Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio
ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashughuri, Shekha Nasser wa
Shear Illusions.
Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail
imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The
Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt,
Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds
Media na Slide Visuals.
Post a Comment