Header Ads

Serikali imetumia Bilioni 459 Kukopesha Wanafunzi wa Elimu ya Juu Mwaka 2015 / 2016

Meneja Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw.Omega Ngole akiwaeleza waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu utolewaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo ambapo jumla ya bilioni 341 zimetolewa.kulia ni Mkurugenzi upangaji na utoaji mikopo Bw.Onesmus Laizer.
Mkurugenzi Upangaji na utoaji wa Mikopo toka Bodi ya Mikopo  kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw.Onesmus Laizer akitoa wito kwa wale wote walionufaika na mikopo kurejesha  ili kupanua wigo wautoaji mikopo hiyo na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu na vyombo vya Habari.

Frank-Mvungi-Maelezo

Serikali imetumia bilioni 459 kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi 122,486 wamenufaika.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.

“Walionufaika na mikopo katika kipindi cha 2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea katika Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi  na haya ni matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano “alisisitiza Ngole
Akizungumzia utolewaji wa mikopo Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na jumla bilioni 341 zilitolewa.

Pia Ngole alibainisha kuwa Serikali imeongeza idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia vipaumbele vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.

Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya awamu ya nne inayosema Hapa Kazi tu.

Aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa kuzingatia sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji mikopo.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi julai, 2005.ambapo Katika mwaka wa Masomo 2005/2006 idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni 56.1 zilitolewa.


No comments

Powered by Blogger.