Header Ads

Serikali inawasaka waliomzulia Rais Dkt JOHN MAGUFULI katika Mitandao ya Kijamii

Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa za uzushi unaosambazwa katika mitandao ya Kijamii ya ndani na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanya biashara hapa nchini kwa kuwa Serikali yake haitataki wageni wafanye bishara zao nchini ambapo  ukweli ni kwamba Serikali haijafukuza wageni wanaofanya biashara zao nchini na haina mpango wa kufanya hivyo kwa wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Serikali.kushoto ni Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya na mwisho kushoto ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Isaac Nantanga,Kulia ni Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.
Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya akitoa wito kwa Watanzania kuwafichua wale wote wanaoingia na kuishi nchini  kinyume cha sheria ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria na kanuni na kusisitiza kuwa Ofisi yake itaendelea kufanya oparesheni ya kuwakamata watu hao, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa na Mwisho Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano Idara ya Habari Maelezo kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ukilenga kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zinasozambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Serikali imewafukuza wafanyabiashara wakigeni wanaofanya kazi zao hapa nchini ,taarifa hizo si za kweli na zinalenga kuichafua  Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na tatizo la wahamiaji haramu , kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa.

(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

No comments

Powered by Blogger.