Header Ads

TIGO KUSAMBAZA MTANDAO WA 4G LTE NCHI NZIMA MWAKA HUU

 2
Ni mtandao wa kasi Zaidi na wenye uwigo mpana Tanzania.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali imetangaza mpango wake wa kupanua huduma ya intaneti ya 4G katika mikoa yote nchini mwaka huu. Huduma hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro, kwa ufanisi na hivyo kuufanya mtandao wa 4G kuwa mpana na wa kasi nchini Tanzania. Ukichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojia ya 4G LTE ina kasi ya nguvu takribani mara tano ikilinganishwa na teknolojia ya 3G ambayo inatumiwa na watoaji wengine wa huduma hiyo kwenye soko la Tanzania. Mtandao wa 4GLTE una kasi kubwa kwenye kurambaza (surf) na kupakua vitu mbalimbali kutoka kwenye intaneti pamoja na kupiga miito ya simu ya skype. Hali kadhalika inawezesha wateja kwa kiwango kikubwa kuwa na uzoefu wa kutiririsha video au kufanya mikutano na inaweza kuhimili kutumika kwenye kupata video, mikutano, muonekano wa hali ya juu, blogu za video, michezo mbalimbali na kupakua video kwenye mitandao ya kijamii.
1
Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo Shavkat Berdiev.
.......
Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo Shavkat Berdiev alisema kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kuwa mipango ya kupanua teknolojia ya 4G hadi kwenye maeneo yote nchini inafanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo ya kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ili kuwawezeshakuendesha maisha ya kidijitali. “Upanuzi wa mtandao wa 4G nchi nzima kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, bali pia kujikita kwake kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwa Watanzania wengi kadri iwezekanavyo,” alisema Berdiev. Tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dola milioni 120 kwa mwaka kwenye upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano. Hali kadhalika kuongeza A idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima. Kwa mujibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) takribaniu asilimia 67 ya idadi ya watu wazima wanamiliki simu za mkononi ambapo idadi ya watumiaji wa intaneti hadi mwaka 2014 ilikuwa imeongezeka hadi kufikia watu milioni 9.3.

No comments

Powered by Blogger.