Header Ads

Wachunguzi wa Urusi wawasili MISRI


Kundi la wachunguzi wa Urusi wamewasili nchini Misri kubaini ni kitu gani kilisabasisha kuanguka kwa ndege ya Urusi katika rasi ya peninsula siku ya Jumamosi ambapo watu wote 224 waliokuwa ndani waliuawa.

Maaafisa nchini Misri na Urusi wamekana madai kutoka kwa kundi la Islamic State kuwa ndilo liliangusha ndege hiyo.


Waziri mkuu nchini Misri Sherif Ismail alisema kuwa tatizo la kiufundi huenda ndilo lilisabaisha kuanguka kwa ndege hiyo.

Vinasa sauti vyote vye ndege hiyo vimepatikana na vitakaguliwa na wachungzui wa Urusi.

Licha ya matamshi hayo mashirika ya ndege ya Emirates, Air France na Lufthansa yamesitisha safari zao katika anga ya Sinai hadi pale habari zaidi zitakapotolewa.

No comments

Powered by Blogger.