Header Ads

Mtoto Mkimbizi Akutanishwa na Familia Yake

Kijana mmoja wa Syria ambaye kutoweka kwake hospitalini mjini Belgrade akiwa katika kambi ya wakimbizi barani Ulaya kulizua hisia kali miongoni mwa mitandao ya kijamii ameunganishwa tena na wazazi wake nchini Ujerumani.

Azama alisafiri mbele ya wazazi wake na mjombaake na alijeruhiwa wakati wa safari hiyo.

Habari yake ilianzisha kampeni katika mitandao ya kijamii yenye alama ya reli Find Azam.Azama hakuwa pekee katika familia hiyo aliyejeruhiwa wakati wa safari hiyo kutoka Syria kuelekea Ulaya.


Kukutanishwa kwake na familia yake siku ya Alhamisi kulifanyika katika hopositali moja ya Ujerumani ambapo babaake anatibiwa mguu wake uliovunjika wakati wa safari hiyo kupitia Ugiriki.

Mvulana huyo alikuwa akilia na uchungu mwingi kwa sababu gari moja lilimkanyaga alipokuwa usingizini ,na hivyobasi kuvunja taya lake.Lakini kabla ya kukamilisha matibabu mjini Belgrade,Azam alipotea na mjombaake.

No comments

Powered by Blogger.