Header Ads

Hivi ndivyo Rais JOHN MAGUFULI alivyopokelewa IKULU siku ya Kwanza !

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wana usalama alipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (Katikati) Akiongozana na Mkewe Mama Janet Magufuli walipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kwenye sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ngoma kama ishara ya kumkaribisha Ikulu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuapishwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaongoza baadhi ya marais wa Afrika Kuimba wimbo wa Taifa, Kushoto kwake ni Rais wa Tanzania aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janet Magufuli na Mke wa Rais aliyemaliza muda wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla iliyofanyika mapema leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ally Mohamed Shein akimueleza jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata wakati wa hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa nchi za afrika na wawakilishi wa mataifa mengine duniani katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Kulia ni Rais aliyemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete na Kulia ni Mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata, Raila Odinga na wake zao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata leo Ikilu Jijini Dar es Salaam.
Raila Odinga akimkumbatia Rais wa Kenya Uhuru Kenyata katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Raila Odinga, na Mama Janet Magufuli akisalimiana na Raila Odinga wakati wa Hafla iliyofanyika Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwaeleza Jambo Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na Rais aliyemaliza Muda wake Dk. Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa awamu ya Pili Alhaj Ally Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)

No comments

Powered by Blogger.