Header Ads

ZIARA YA KATIBU MKUU WA, KOMREDI ABDULRAHMAN KINANA INAENDELEA MKOANI KAGERA



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasomea wananchi wa kijiji cha Nkwenda vijiji vitakavyopata umeme wa mradi wa umeme vijijini katika wilaya ya Kyerwa,mkoani Kagera.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Nkwenda na kuwaambia kuwa Chama Cha Mapinduzi ni chama pekee chenye sera zinazomgusa kila mwananchi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Kyerwa Bw.Eustace Katagira mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji cha Nkwenda.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella mara baada ya kumaliza kuwahutubia wakazi wa kijiji cha Nkwenda.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kahawa iliyopo shambani pamoja na Mkulima mwenye shamba hilo Ndugu Eustace Kubalienda Kishunji ambaye ana miche 345 ambayo huvuna magunia 25 na ana shamba la migomba ambalo huvuna mikungu 45,
Mzee Kishunji ambaye anaishi katika kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira ameweza kusomesha watoto wawili katika vyuo vikuu vya Dar es salaam na Dodoma.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira wilaya ya Kyerwa.

 Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kikukuru kata ya Mabira wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya Zahanati ya kijiji cha Kigorogoro kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Dk. Mohamed Kassim Mpunjo


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kigorogoro wilaya ya Kyerwa.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kigorogoro ambapo alisema serikali irahisishe taratibu za wakazi wa mipakani kupata huduma na mahitaji nchi jirani pamoja na kupunguza vikwazo vya biashara kwa wananchi wa mipakani.

 Soko la Kimataifa la Murongo likiwa limesimama ujenzi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Murongo ambapo aliwaambia miradi inayoanzishwa vijijini isisimamiwe na watu wa Dar es salaam na badala yake isimamiwe na Manispaa husika.

 Wananchi wa kijiji cha Kibingo kata ya Kaisho wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amesimama kwenye gari ya Katibu Mkuu wa CCM kuangalia mkutano unavyoendelea.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia  wakazi wa Kibingo na kuwaambia atasaidia kusukuma mabadiliko katika soko la Kahawa.

 Wananchi wa kijiji cha Kibingo kata ya Kaisho wilaya ya Kyerwa wakiaga msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

 Wapenzi na wanachama wa CCM wakicheza ngoma ya asili wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera akiwasalimu wananchi wa Isingiro, wilaya ya Kyerwa.

 Mbunge wa Kyerwa Bw.Eustace Katagira akihutubia wananchi wa Isingiro kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Isingiro 

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Isingiro, wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.

(Picha zote na Adam Mzee)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

No comments

Powered by Blogger.