Baadhi ya wachezaji wa Serengeti Boys wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Hayupo Pichani) katika hafla fupi kabla ya mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville itakayofanyika katika Uwanja wa Taifa Septemba 18,2016.
Na Shamimu Nyaki- WHUSM
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa kiasi cha shilingi million tano kwa timu ya Serengeti Boys kama motisha katika mchezo wao dhidi ya Congo Brazivile utakayochezwa leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.
Akikabidhi pesa hizo leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Nape amewataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 .
“Watanzania wote tupo pamoja na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili, Sisi kama Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia heri ili mlete heshima kwa Taifa.”Alisema Mhe. Nape.
Kwa upande wa Kocha wa Timu hiyo Bw.Bakari Shime amemuhakikishia Waziri na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.
Aidha Nahodha wa Timu hiyo Bw. Issa Abdi Makame mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo kutoka Bechi la ufundi ili kuhakikisha wanapata ushindi.
“Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.
Timu hiyo ya vijana chini ya umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwaka 2017.
|
Post a Comment