Shule za Fedha sasa Kufunguliwa Jijini Mwanza
Kutoka kushoto ni balozi wa shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi ya Time To Help, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza na Meneja wa Shule za Feza mkoani Mwanza, Metin-Er.
Uongozi wa Shule za Feza (Feza Schools) nchini Tanzania mwakani unatarajia kufungua tawi la shule hizo Jijini Mwanza, ili kuendelea kufikisha karibu upatikanaji wa elimu karibu na jamii nchini.
Balozi wa shule hizo mkoani Mwanza, Faisal Hafidh na Taasisi ya Time To Help (kushoto), aliyasema hayo juzi jumatatu Septemba 12,2016 wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa mboga (nyama) kwa makundi mbalimbali ya wahitaji mkoani Mwanza kama sehemu ya kusherehekea Sikukuu ya Eid El Hajj.
Alisema lengo la Shule za Feza kwa kushirikiana na taasisi yake ya Time To Help ni kusaidia jamii ya watanzania bila kujali dini, kanila wala mipaka ya aina yoyote.
Msaada uliotolewa na Shule za Feza ni nyama kilo 500 ambazo ziligawiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye Kituo cha Wazee Bukumbi, Bakwata mkoani Mwanza, Taasisi za Juqusuta, Ummy Salama na Masjid Noor Mahina.
Msaada wa mboga uliotolewa Shule za Feza mkoani Mwanza.
Shule za Feza zinapatikana katika mataifa mbalimbali duniani ambapo nchini kuna tawi Jijijini Dar es salaam na sasa mkakati ni kufungua tawi mkoani Mwanza.
Post a Comment