Mbunge RIDHIWANI asaidia Matibabu ya Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo Wazi
Mbunge wa Chalinze akiwa katika wodi ya watu waliopata ajali na matatizo mengine ya viungo wakisubiri kupatiwa huduma na wale waliopatiwa huduma ya mifupa kuwajulia hali na kuwapa pole.
|
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani kikwete akipata maelezo toka kwa madaktari wa Moi waliokuwa wanawapokea na kuwaaangalia watoto walikua na matatizo. |
Mbunge Ridhiwani akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ufungaji wa mafunzo ya usalama wa barabarani kwa waendesha bodaboda wa Wilaya ya Chalinze.
|
Baadhi ya vijana waliofuzu mafunzo na kupatiwa leseni ya udereva wa bodaboda msaada wa Ofisi ya Mbunge wa Chalinze wakifuatilia kwa makini yanayotokea katika kikao hicho. |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ameshirikiana na Gsm Foundation na MOI kusaidia kutibu watoto nane wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Katika matibabu hayo watoto wapatao 23 walifanyiwa vipimo na 8 kati yao walikutwa na matiatizo hayo na kufanyiwa upasuaji,na kuongeza kuwa watoto wengine walikutwa na matatizo tofauti na hayo,na kupelekwa katika hosptali ya taifa Muhimbili na wengine walipelekwa kwa madaktari bingwa wa magonjwa kwa matibabu.
“Watoto wote waliofanyiwa operesheni tuliwakuta wanaendelea vizuri wakiwa na wazazi wao wakiendelea kuwapatia huduma za mwisho kabla ya kuruhusiwa”,alisema Kikwete.
Aidha,Mbunge huyo amewaomba wazazi kutowaficha watoto wenye matatizo kama hayo kwani yanatibika na kuacha kuendekeza Imani potofu za kuwafungia ndani na badala yake kuwapeleka katika vituoa vya afya ili kupata matibabu.
“Nawashauri wazazi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo kwa kufanya hivyo ni kuwanyima watoto nafasi ya kupona na kuishi maisha kama watoto wengine”,alisema Kikwete.
Kikwete amewaomba wadau katika sekata ya afya kujitokeza kuungana na Gsm Foundation katika kusaidia katika sekta hiyo ili kumkomboa mtanzania kuondoka na matatizo ya kiafya yanayowakabili.
“Nawashukuru sana Gsm kwa kujitoa kusadia watoto hawa kupata matibabu kwa ni jambo la kupigiwa mfano na wadau wengine katika kusaidia jamii”,alisema Kikwete
Mbunge huyo ameshukuru madaktari kwa kujitolea muda wao na kuwatibu watoto hao na kutoa wito kwa Gsm Foundation kuondelea kusaidia katika Mkoa wa Pwani ili kuwafikia watoto wengine katika maeneo ya Mkuranga,Kibiti,Mafia na Rufiji.
Katika hatua nyingine Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa polisi Mkoa wa Pwani,polisi Wilaya ya Chalinze na kituo cha udereva wa vyombo vya moto cha Winners Driving School wameendesha mafunzo ya udereva kwa vijana 160.
Mafunzo hayo ya udereva yamewezesha vijana hao kupatiwa leseni mara baada yakumaliza mafunzo yatakayo wasaidia katika shughuli zao za kila siku za kujitafutia kipato,mafunzo hayo yamegharimu shilingi milioni 20.
Post a Comment