Kumbukumbu ya Kifo cha Mwanahabari DAUDI MWANGOSI, UTPC yalilia Mazingira Huru
Septemba 2,2012 Mwandishi wa Habari, Marehemu Daudi Mwangosi (hayuko pichani), aliyekuwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Iringa, aliuawa na polisi akiwa kazini katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ambapo aliyemuua alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani julai mwaka huu.
Kufuatia mauaji hayo, Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini, UTPC ulitenga tarehe hiyo kuwa kumbukumbu ya Kifo cha Daudi Mwangosi ikiambatana pia na tuzo inayotolewa kwa mwanahabari aliyefanya kazi katika mazingira magumu ikiwemo kupigwa ama kuuawa kutokana na kazi yake.
Leo UTPC imekutana na wanahabari Jijini Mwanza imekutana na wanahabari ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Mwangosi ambapo imelaani mazingira magumu ambayo wakati mwingine wanahabari na vyombo vya habari wanayapitia katika utendaji wao wa kazi ikiwemo vyombo vya habari kufungiwa.
Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) amesema wanahabari wanataka mazingira huru ya kufanya kazi huku akilaani serikali kuvifungia baadhi ya vyombo vya bila kusikilizwa juu ya yale yanayodhaniwa kufanywa na vyombo hivyo kinyume cha sheria.
Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji .
Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, amebainisha kwamba tunzo ya Daudi Mwangosi mwaka huu pia haikupata mshindi kwa namna ambavyo jopo la tuzo hiyo lilivyoweka vigezo vyake ikiwemo Mwandishi anayepaswa kuichukua awe amepigwa, kuumizwa ama kuuawa akiwa kazini. Mwaka 2013 tuzo hiyo ilichukuliwa na Mwanahabari Absolum Kibanda.
Vingozi wa UTPC wakimkumbuka marehemu Daudi Mwangosi.
Wanahabari mkoani Mwana wakimkumbuka marehemu Daudi Mwangosi.
Post a Comment