Kiwanda cha Saruji Chaipiga Tafu Sekondari ya Ilboru ARUSHA
Tanga,
KIWANDA
Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya
Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya
milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.
Akizungumza wakati wa
halfa fupi ya
makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto
za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.
Alisema msaada huo
utapunguza uhaba
wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza
kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika
ipasavyo.
‘Mifuko hii ya saruji
itapunguza changamoto
inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba
vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu”
alisema Malambugi.
Mkuu wa Idara ya
Rasilimawatu
kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi,
akimkabidhi mifuko
ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya
Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa
ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma
kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas
mhasibu.
Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.
Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.
Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.
‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla.
Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.
Post a Comment