Washiriki 15 Wachaguliwa Katika Shindano la TIGO DIGITAL CHANGE MAKER'S 2015
Baadhi ya washindi wa shindano la Tigo Changemakers katika miaka ya hivi karibuni wakipokea hundi zao dola 20,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez.
...............................
...............................
Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Reach for Change (R4C)
wametangaza washiriki 15 wenye vipaji
vya ujasiriamali wa kijamii wamechaguliwa katika shindano la “Tigo Digital Change Makers’ ambapo washindi
wawili watatangazwa wiki ijayo.
Shindano hili lilioanza
Septemba, limepokea mamia ya maombi kutoka kwa washiriki wenye ubunifu wa kiteknologia
katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, ukulima na afya kwa mujibu wa Afisa wa
Huduma kwa Jamii wa Tigo, May Thomas.
Katika taarifa
iliyotumwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salam leo, May amesema, wajasiriamali
wa kidijitali 15 waliochaguliwa kila
mmoja wao alileta suluhisho la kidijitali lenye ubunifu lilokusudia kuboresha
maisha ya watoto nchini Tanzania, na ndio kigezo kilicho wafanya wafuzu
kushiriki katika shindano hilo.
May alisema: wengi
katika hawa waombaji fikra zao bunifu zimeenda sambamba na mkakati wetu wa
kuleta mabadiliko ya kidijitali maishani. Hali imesababisha changamoto kubwa
katika zoezi la kuchagua washindani,” alisema, huku akiongeza kuwa washindi hao
wawili watapokea dola za
kimarekani 20,000 kila mmoja kwa ajili ya kutekeleza miradi yao.
Tigo na Reach for
Change wameendesha shindano hili la Digital Change-Makers nchini Tanzania kwa
kipindi cha miaka mitatu sasa, ambapo wajasiriamali wa kijamii saba wameshinda fedha kwa ajili ya kutekeleza
miradi yao. Kwa mujibu wa May, miradi ya wajasiriamali wa kijamii hao saba kwa
pamoja imesaidia zaidi ya watoto 10,000 nchini katika kipindi hicho.
Shindano la Tigo Digital –Makers lina malengo ya kuwaendeleza na kuwatia
moyo wajasiriamali wa kijamii kutumia teknolojia za kidijitali kusuluhisha
baadhi ya matatizo sugu nchini Tanzania.
Post a Comment