Wafanyakazi wa NURU FM 93.5 Iringa Wafanya Usafi Hospitali ya Mkoa huo
Fredy mgunda ambaye ni chief repoter wa radio nuru fm.
hawa muhamed na devota romanus wakiwa eneo la tukio wakifanya usafi.
shauri mkwawa a.k.a mama la mama na wafanyakazi wenzake wakifanya usafi.
shauri mkwawa a.k.a mama la mama na wafanyakazi wenzake wakifanya usafi.
Wafanyakazi wa kituo cha redio nuru fm 93.5 iringa wamejitokeza
kufanya usafi katika hospital ya rufaa ya iringa kwa lengo la kumuunga mkono
rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dr john pombe magufuli.
Wakizungumza wakati wakiwa wanafanya usafi katika
eneo hilo wamesemakuwa wameamua kufanya usafi katika hospital hiyo kwa kuwa
ndio hospital inayohudumia wananchi wengi kuliko hospitali nyingine zilizopo
mkoani hapa.
Denis nyali ni mhariri wa habari wa radio hiyo
amesema kuwa wameamua kufanya usafi kwa lengo la kuwaonyesha wananchi na
wafanyakazi wa hospital hiyo kuwa iringa kuwa safi inawezekana kutokana na
kauli moja tu aliyoitoa rais imekuwa gumzo kila kona hivyo wananchi wanatakiwa
kufanya usafi kila mara na usafi uwe jadi yao.
“Angalia hapa leo hospitali kama hii ya rufaa uchafu
wote huu unatoka hapa kama wanagekuwa wanafanya usafi kila siku na kuona usafi
ni sehemu ya maisha yao tusingeona hali hii na pia tusinge pata wagonjwa wa
magonjwa ya milipuko naomba wananchi wezangu zoezi hili liwe endelevu”alisema
denis nyali.
Hawa muhamed na grace michaeli wamesema ni aibu
wananchi kukumbushwa kufanya usafi na rais wakati huo ni wajibu wa kila
mwananchi na kuongeza kuwa wanampongeza rais wa awamu ya tano kwa kasi yake anayoendana nayo sasa kwa
inawafanya watanzania waanze kuiamini serikali yao tofauti na ilivyo kuwa hapo
awali.
Fredy mgunda ambaye ni chief repoter wa radio nuru
fm amewataka wananchi kuendeleza juhudi za rais kwa kuwa wasafi kila siku na
kuafanya usafi kila mara ili nchi hii isikumbwe na magonjwa ya milipuko na
kuongeza kuwa serikali ya manispaa ya iringa inatakiwa kutunga sheria
ndogondogo za usafi.
“Hapa iringa hatuna kabisa sheria za usafi kwa
utaona wananchi wanatupa takataka hovyo huku viongozi wa mji huu wakiwa kimya
kwa namna hiyo hatuwezi kuwa na mji msafi hata siku moj,ukienda pale stand watu
wanakojoa na kujisaidia hovyo lakini hawachukuliwi hatua yoyote ile “alisema
fredy mgunda
Hussein faraha ni mtangazaji wa radio hiyo amewaomba
wananchi kuendeleza kufanya usafi kwa kuwa ndio jadi ya mtazania hata
ukikumbuka hapo zamani wakati mwalimu nyerere akiwa hai alikuwa akisisitiza
usafi hivyo ujio wa rais huyu wa awamu ya tano john magufuli naanza kufananisha
na marehem waziri mkuu Edward molinge sokoine kwa uchapaji kazi wake.
“Leo nimemuana rais huyu akizama kwenye matope
kufanya usafi huku akiwa na sura ya furaha kujumuika na wananchi wakati wa
kufanya kazi hiyo ni ishara tosha kumlinganisha na marehemu mwalimu nyerere
kwani alikuwa anafanya kazi pamoja na wananchi wake”. alisema husien farahani
Naye jeni kalinga amesema kwa anamkubali sana rais
kwa kasi yake na kuwaomba wananchi kumuombea awe na uhai kwa kuwa sasa
anatimiza matakwa ya watanzania wengi waliokuwa wamekata tamaa na nchi yao
“Daa jamaa yangu magufuli jembe kinoma si unaona
linavyolima kila kona ni gumzo hivyo lazima tumpe nguvu na serikali imuongezee
ulinzi tuiseje tukalipoteza jembe letu lilorudisha matumaini ya watanznia”alisema
jeni kalinga.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo
wamekipongeza kituo hicho cha radio kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa
wamejituma kufanya usafi kwenye mahodi na nje ya hodi hasa wanaume walikuwa
wanadeki huku kwenye mahodi hicho ni kitendo cha kujivunia kutoka kwako.
Post a Comment