Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie
Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi wa
Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi
(kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo
Desemba 11, 2015.
...................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana
amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo
yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya
maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga
kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
Katika
hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake
Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani
na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini
Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi
hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
Imetolewa
na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu,
Dar es Salaam
| | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | | |
Post a Comment